杏MAP导航

Tafuta

2025.06.12 VI: Mkutano wa Njia Mpya za Maisha ya Wakfu huko Mtakatifu Anselmo. 2025.06.12 VI: Mkutano wa Njia Mpya za Maisha ya Wakfu huko Mtakatifu Anselmo. 

Waliowekwa wakfu kufungua safari,kati ya jumuiya mpya na mizizi ya kizamani

Kuanzia tarehe 12 hadi 14 Juni 2025 katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Anselmo unafanyika Mkutano wa VI aina za maisha ya kitawa.Tukio lililohamasishwa na Jumuiya zinazotambulika za kikanisa kwa kujadili utambulisho,utume na mitazamo ndani ya Kanisa la kisinodi,katika mazungumzo na Vatican.

Na Eleanna Guglielmi – Vatican.

Maisha ya wakfu yanaendelea kujitafakari  juu ya namna ambavyo Injili inavyomwilishwa leo hii, kati ya uaminifu kwa mapokeo na uvumbuzi unaovuviwa na Roho Mtakatifu. Tangu 2011, mfululizo wa mikutano wenye kauli mbiu: "Aprendo Cammini" yaani “kufungua njia” umekuwa ukiunda nafasi ya mazungumzo kati ya taasisi za maisha ya wakfu na Jumuiya mpya ambazo, licha ya utofauti wao wa karama, zinashiriki nia njema ya kutembea pamoja katika Kanisa. Kwa njia hiyo ikiwa ni Mkutano wa sita unafanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Juni  2025 kwenye Ukumbi wa Chuo cha Kipapa cha Mtakatifu Anselmo, jiji Roma kwa kuendeleza safari hii ya Ushirika kwa kutoa jukwaa la kikanisa la majadiliano na utambuzi, kusikiliza Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maisha ya Kitawa na Vyama vya Kitume.

Mkutano wa watawa 12-14 Juni 2025
Mkutano wa watawa 12-14 Juni 2025

Kati ya utambuzi wa kisheria na safari ya sinodi

Mkutano huo unaorudiwa kila baada ya miaka mitatu, unalenga kuwa nafasi wazi kwa hali halisi ambayo tayari imetambuliwa na ile ambayo bado inatafutwa. Wengine bado ni wachanga sana na wako kwenye njia ya kutambuliwa kikanisa, wengine tayari wameidhinishwa na mamlaka ya kikanisa. Kwa sababu hiyo, moja ya malengo makuu ya mkutano huo ni kutafakari juu ya sinodi, juu ya uhusiano kati ya karama na uongozi na juu ya utambuzi wa kikanisa kwa kuzingatia hati za hivi karibuni, Mahusiano ya Kawaida, umoja na uwajibikaji wa pamoja.

Tukio linalofungamana na mapokeo na unabii

Tukio hili lililoandaliwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Kimonaki ya Athenaeum ya Kipapa ya Mtakatifu Anselmo, linajumuisha michango kutoka kwa wataalamu, waamini na wawakilishi wa ulimwengu wa kikanisa. Wazungumzaji ni pamoja na Padre Leonello Leidi, wa Baraza la Kipapa la Maisha ya Kitawa na Vyama vya Kitume; Lourdes Grosso, mmisionari idente wa Taasisi ya Id ya Kristo Mkombozi, mshauri wa Baraza hilo; Padre Mbenediktini Fernando Rivas, mkuu wa Taasisi hiyo ya Kimonaki; Sr Patrizia Girolami, Mcistercian wa Valserena. Mazingira ya Wabenediktini ambamo mkutano unafanyika huchangia katika ulinganisho na mazungumzo kati ya riwaya ya karama zinazoibuka na uimara wa mapokeo ya kimonaki, kwa nia ya kutajirishana.

Mkutano wa watawa 12-14 Juni
Mkutano wa watawa 12-14 Juni

Kuelekea Kanisa linalotembea pamoja

Siku za vikao hivyo vya jumla vinahusisha  kazi ya vikundi na wakati wa sala ya pamoja. Jumamosi tarehe 14 Juni 2025 kwa kuwa na meza ya pande zote juu ya matarajio ya maisha ya wakfu katika Kanisa leo hii. Mwishoni mwa mkutano, itafanyika hija  ya Jubilei kwa miguu kuelekea Kanisa Kuu la  Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta ambayo ni  ishara inayoonekana ya hamu ya kupita kwenye milango ya wakati huu pamoja na mitazamo yetu kuelekea ushirika na utume.

13 Juni 2025, 12:16