Vurugu zisizoisha:Wamisionari Wabenediktini wafunga vituo vyao katika Kerio Valley
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Masista Wamisionari Wabenediktini wa Kipaumbele cha Moyo Mtakatifu wamefunga vituo vyao vyote huko Kerio Valley, nchini Kenya, kufuatia vitendo vya ukatili vinavyoendelea kutokea kila siku katika eneo hilo. Wamisionari wenyewe, kupitia barua iliyotolewa kwenye chaneli zao za mitandao ya kijamii, walitangaza, "pamoja na mara moja", kufungwa kwa misheni hiyo "kwa muda usiojulikana."
Uamuzi wa kufunga vituo
Uamuzi huo, unasomeka kwa maandishi yaliyotiwa saini na Sr a Rosa Pascal OSB, Mkuu wa Masista Wamisionari Wabenediktini, ulichukuliwa “kufuatia na mauaji ya Padre Alloy Bett, Paroko wa Mtakatifu Mathias Mulumba na kuendelea kukosekana kwa utulivu katika eneo hilo. Hili limeathiri vibaya kazi yetu ya umisionari” na kusababisha “uchungu wa kiakili, kihisia na kisaikolojia kwa dada zetu” na, kwa sababu hiyo, “kutowezekana kutekeleza huduma muhimu kwa sababu ya ukosefu wa wafanyakazi ambao wanatelekeza eneo hilo,” kwa hivyo uamuzi wa "kufunga vituo vyetu vya misheni kwa muda usiojulikana, hadi eneo liwe salama kwa huduma." Hatua hii, inabainisha taaifa hiyo, "inalenga kuhakikisha usalama wa dada zetu wanaofanya kazi katika mkoa, wafanyakazi wetu na wale wanaotembelea misheni yetu kwa huduma mbalimbali", wakati huo huo, "kuitaka serikali kutafuta suluhisho la kudumu la amani katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na kuwapokonya silaha raia."Miongoni mwa vituo vilivyofungwa pia ni Hospitali ya Misheni ya Chesongoch.