杏MAP导航

Tafuta

2025.06.11:Sr Veronica Donatello alizungumza katika Umoja wa Mataifa katika Mkutano wa 18 wa Mwaka wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu. 2025.06.11:Sr Veronica Donatello alizungumza katika Umoja wa Mataifa katika Mkutano wa 18 wa Mwaka wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu. 

Ulemavu,Sr, Donatello katika UN:fursa za AI na ugumu katika mazingira ya vita!

Hotuba ya mtawa wa Kifransiskani ambaye ni mkuu wa Huduma ya Kichungaji ya Watu Wenye Ulemavu kwa CEI na mratibu wa mpango wa"Hakuna Aliyetengwa"unaohamasishwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano katika Mkutano wa 18 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (COSP) ambao ulifungwa tarehe 12 Juni 2025 huko New York Marekani."Mimi ndiye mtawa pekee,watu wana hamu ya kujua na kushangazwa na kazi ya Kanisa katika uwanja huu.Tunachangamoto potofu na chuki."

Na Antonella Palermo na Angella Rwezaula - Vatican.

Kufahamisha kujitolea kwa Kanisa nchini Italia na Vatican kwa ajili ya kujumuika. Hili ndilo lengo kuu la hotuba ya Sr  Veronica Donatello, mkuu wa Huduma ya Kitaifa ya Kichungaji ya Watu Wenye Ulemavu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Nchini Italia (CEI) na mratibu wa Mpango  wa "Nessuno Escluso" yaani “hakuna aliyetengwa” unaohamasishwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano katika kikao cha 18 cha Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu(COSP) ulioanza tarehe 10 Juni na kumalizika tarehe 12 Juni 2025 huko mjini New York, Marekani. Mada ya jumla ya tukio hilo la siku mbili lilikuwa ni  kuimarisha uelewa wa umma juu ya haki na michango ya watu wenye ulemavu kwa ajili ya maendeleo ya kijamii kwa kuzingatia Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Maendeleo ya Jamii unaotarajiwa kufanyika mnamo(Novemba 2025).

Matarajio ya kuingizwa katika kila umri na hali

Sr Veronica wa Shirika la Kifransiskani kutoka Alcantara akihojiana na vyombo vya habari vya Vatican alisema kuwa " ilikuwa ya kufurahisha kuwa hapa kwa utajiri wa kulinganisha na mataifa mengi," huku akisisitiza umuhimu wa kuwafanya watu kuelewa mbinu inayozidi kulenga kusindikizana na watu wenye ulemavu "katika kila hali na katika kila umri wa maisha, kwa kuzingatia kusaidia familia, kujua jinsi ya kufanya kazi katika uwanja wa kiroho, katika uwanja wa mabadiliko ya maisha. Na juu ya yote katika mazingira mbalimbali ya maisha, na mazingira ambayo yana changamoto. Mabadiliko yetu ya dhana ni juu ya kiutamaduni,” Alisisitiza. “Baada ya hotuba, wengi waliniambia: 'Ni ajabu jinsi gani, hatukufikiri kwamba Kanisa linafanya haya yote!' Hili ni jambo la kufurahisha kwa sababu hatua kwa hatua tunapinga baadhi ya dhana potofu, ya  chuki fulani na ambayo Injili ilifanya na kuleta mapinduzi."

Sr Veronica Donatello akizungumza katika Umoja wa Mataifa
Sr Veronica Donatello akizungumza katika Umoja wa Mataifa

Umuhimu wa majadiliano

Kuwa mtawa pekee katika mkusanyiko huo wa kimataifa ni muhimu: "Inapendeza sana kwa sababu ninapata tabasamu nyingi, watu wananiuliza ninafanya nini hapa, au ikiwa tayari nimekutana na Papa mpya. Kuna udadisi na matarajio mengi. Kuna kazi muhimu ambayo Vatican imejaribu kutekeleza katika miaka ya hivi karibuni ili kupambana na kutengwa na upweke ambao unatambuliwa. Kwa njia hiyo, tunaweza kusema, mikutano baina ya nchi mbili huzaliwa kwa sababu tunataka kujadili masuala fulani pamoja." Kusikiliza ni jambo la msingi, kwa mujibu wa Sr Veronica, ambaye ameguswa zaidi na mchango wa Akili Nunde(AI) kwa kazi ya kichungaji, na uhamiaji ambapo jambo hili linapandikizwa kwenye masharti ya ulemavu, na kusababisha matatizo mengine kutatuliwa.

Sr Donatello anaamini, kama wengi, kwamba teknolojia mpya zinatoa mchango muhimu, hasa kutoka Asia, kuboresha ubora wa maisha: "Lakini kamwe hatupaswi kusahau kwamba mwishowe kuna mtu." Na pia aliakisi kusikitishwa kwa pengo kati ya mipaka ambayo sayansi inaongoza kwa haraka na ugumu ambao familia nyingi hupata, hasa katika mazingira ya vita, kwa mfano Amerika ya Kusini, na barani Afrika. "Ni ugumu wa kuweza kudhamini haki za chini kabisa za maisha, zile ambazo unachukuliwa kuwa mtu. Ni lazima tuondokane na pengo hili kubwa." Si ya kupuuzwa, basi, ni hali ngumu sana ambapo aina ya "kubaguliwa mara tatu" inaonekana: hizi ni kesi ambapo mhusika ni mwanamke mgeni mlemavu. Hapa changamoto inafikia viwango vya juu sana na majibu ya kutosha ya kichungaji yanahitaji kiasi sawa cha mafunzo na uvumilivu. Kazi na mpango wa "Vatican kwa wote", juu ya upatikanaji wa matukio ya Papa, ni kati ya mifano ambayo Sr Donatello alishirikisha katika hotuba yake katika Umoja wa Mataifa ambapo alionesha umuhimu wa kukuza kazi, muda wa kujitolea, michezo, hotuba, sanaa na elimu katika upendo.

Kuwa na uelewa wa wenye matatizo ya ulemavu
Kuwa na uelewa wa wenye matatizo ya ulemavu   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Locatelli: kutoka kwa ustawi hadi ushujaa

Hizi zilikuwa siku kali kwa Italia katika Umoja wa Mataifa, ambapo, kama Waziri wa Ulemavu Alessandra Locatelli wa Italia aliviambia vyombo vya habari vya Vatican, kwa sababu ilishiriki katika kikao cha COSP. Hapa aliweza "kushuhudia dhamira kuu ya mageuzi ya walemavu lakini pia kwa mabadiliko katika mtazamo: kutoka kwa maono ya ustawi hadi maono ya kuthaminiwa kwa uwezo, talanta na ujuzi". Locatelli alisisitiza umuhimu wa njia za mawasiliano na lugha zinazoshughulikia masuala haya: "Usioneshe ulemavu tu wakati kuna matukio ya kutisha au mazuri, lakini sema historia ya maisha ya kila siku", ni tumaini lake. Miongoni mwa matukio ya kipekee yaliyoandaliwa na wajumbe wa Italia, bendi katika tamasha na mkutano na vyama vingi na mashirika ya burudani na uwakilishi wa Sekta ya Tatu. Hivi ndivyo kazi ya maandalizi ya G20 ambayo itafanyika Afrika Kusini mwaka ujao 2026, imepata nafasi, na ambayo inakusudiwa kuwa katika mwendelezo wa kazi ya G7, ya kwanza katika historia inayojitolea kwa walemavu, iliyofanyika mwaka 2024 huko Assisi.

Kuwezesha watu wenye uliemavu na kuimarisha sera za maendeleo yao kijamii

Mkutano wa Nchi Wanachama ni tukio la kila mwaka linaloandaliwa na Umoja wa Mataifa. Katika Mkutano huo, washiriki walijadili utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu. Washiriki ni pamoja na wawakilishi wa Nchi Wanachama (nchi na mashirika ya kikanda ambayo yaliidhinisha Mkataba), mashirika ya kiraia (kama vile mashirika ya watu wenye ulemavu) na wataalam wa haki za ulemavu (kama vile Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wenye ulemavu na wasomi). Katika kikako cha 18 cha Mkutano wa Nchi Wanachama kwa CRPD ya Umoja wa Mataifa (COSP17) kimefanyika  kuanzia tarehe 10-12 Juni 2025 mjini New York. Mada kuu ni “Kukuza uelewa wa umma kuhusu haki na michango ya watu wenye ulemavu kwa ajili ya maendeleo ya kijamii kuelekea Mkutano wa Kijamii wa Dunia.” Mada ndogo  zilikuwa tatu:1: Kuwawezesha watu wenye ulemavu na kuimarisha sera za maendeleo ya kijamii kupitia ufadhili wa kibunifu. Ya 2: Kutomwacha yeyote nyuma: kutumia Akili Nunde (AI) kama zana ya kusaidia ujumuishi ili kuimarisha ushiriki wa watu wenye ulemavu. Na ya 3: Kutambua na kushughulikia haki za watu wa kiasili wenye ulemavu na jukumu lao katika kuendeleza ujumuishaji wa ulemavu.

13 Juni 2025, 12:27