Karama ya Mtakatifu Rita katika kazi zilizozaliwa baada kutangazwa kwake kuwa Mtakatifu
Na Tiziana Campisi – Vatican.
Basilika ya Mtakatifu Rita, Basilika ya Chini, eneo la kuungamia, monasteri ya watawa wa Kiakogostini hayo yote yapo Cascia, mji mdogo katikati ya Mkowa wa Umbria, ni sanduku la hazina la maeneo ambayo huhifadhi kurasa za thamani za historia, kutoa nafasi kwa sala na kiroho na kukaribisha mahujaji na waamini kila siku. Watawa Konventi ya Mtakatifu Agostino wanajitoa kwa ajili ya uchungaji wao, wakiungwa mkono mwaka mzima na makumi ya waungamisho ambao ni mapadre wa kutoka mataifa mbalimbali ambao mara kwa mara hubadilishana na wengi wao hutoka katika vyuo mbalimbali vilivopo Roma.
Ushirika na ukweli wa vyama vya tasaufi ya Agostino
Na kisha kuna ukweli mwingine mwingi: Mfuko wa Mtakatifu Rita wa Cascia, ambao unatunza kazi za upendo na mipango ya mshikamano ya Monasteri ya Mtakatifu Rita; Kioto(L'Alveare,) nyumba ya malazi na elimu kwa watoto wa kike na wasichana(La apette) kutoka katika familia zilizo katika shida lakini pia nafasi iliyo wazi kwa watoto wadogo(millefiori) kwa shughuli za elimu na burudani. Si hiyo tu pia Chama cha waacha Mungu cha Mtakatifu Rita, ambacho ni cha kiagostino kinacholeta pamoja wale wanaomtafuta Mungu, kwa kufuata nyayo za Mtakatifu Agostino na Rita, kukuza tunu za familia, amani, msamaha na upatanisho, kueneza ibada na ibada ya Mtakatifu Rita, kwa kushirikiana na shughuli na mipango ya Basilika, monasteri ya Waagostiniani wa Kike na Kiume kwa pamoja.
Mahujaji kutoka pande zote za dunia
Maisha ya kila siku huko Cascia yanajumuisha mikutano, maadhimisho ya misa, nyakati za sala na watu kutoka pande zote za dunia, anafafanua kwa vyombo vya habari vya Vatican Padre Juraj Pigula, Mkuu wa Conventi ya Agostino. Baada ya kutangazwa kuwa mtakatifu mnamo tarehe 24 Mei 1900, wakati wa Papa Leo XIII, umaarufu wa mtakatifu wa kesi zisizowezekana ulieenea katika mabara yote na leo hii wengi wanakwenda hkumwomba kutoka Lebanon, Ufilipino, India, Brazil, Poland na nchi nyingine ambako hakujulikani sana, kama vile Kroatia, Slovakia, Jamhuri ya Czech. Alisema Padre Juraj, lakini pia mahujaji wanatoka Afrika na Australia. Kwa ufupi, “Mtakatifu Rita hupita katika utakatifu wake hasa kwa ajili ya hali yake ya kiroho iliyo sahihi sana, kwa sababu yeye ni mwanamke wa amani, anayetufundisha kusamehe na kumtumaini Mungu daima, kusali bila kukoma, bila kukata tamaa."
Kwa upande wa Padre Juraj, maadhimisho ya miaka 125 tangu kutangazwa kwake kuwa Mtakatifu, yaliyoadhimishwa Jumamosi tarehe 22 Mei 2025, ilizindua upya ujumbe wake wa amani na anatualika kugundua upya mtindo wake wa maisha ambao kila mtu anaweza kuuiga, kwa sababu, kama Mtakatifu Rita, sote tuna matatizo katika mahusiano, tunakasirika, wakati mwingine hatuongei sisi kwa sisi katika familia, hasa kwa masuala mbalimbali na kwa hiyo daima kuna haja ya upatanisho.” Zaidi ya hayo, Mtakatifu Rita alikuwa mama, na kwa hiyo anapendekeza hata leo jinsi ya kuelimisha watoto, na kisha njia ambayo alikabiliana na mateso inatufundisha kuteseka kwa upendo, si kwa kunung'unika, bali kwa kubadilisha maumivu," alisema Padre huyo.
Kazi ya Mama Maria Teresa Fasce
Pamoja na hayo pia kuna historia ndani ya historia huko Cascia. Si kila mtu anajua kwamba katika Basilika ya Mtakatifu Rita shukrani kwa Mama Maria Teresa Fasce kutoka Liguria, ambaye alikuwa ni Mama Mkuu wa Monasteri ya Mtakatifu Rita kwa miaka 27, kuanzia mwaka 1920 hadi 1947, alisema Padre Pietro Bellini, anayehudumia kwenye Sakristi. Wito wake unahusishwa na kutangazwa kuwa Mtakatifu Rita. Alikuwa na umri wa miaka 19 wakati huo, habari hiyo ilimtambulisha kwa Mtakatifu wa kiagostini, alivutiwa naye na aliamua kujitoa kwa Bwana kama yeye, katika nyumba ya watawa ambako aliishi.
Wakati huo Cascia ilikuwa kijiji kidogo cha wakulima, alieleza Padre Pietro, kwamba katika jumuiya ya watawa kulikuwa na watawa wachache wa kitawa, na pengine walikuwa na elimu duni, labda wanaoishi katika umaskini.” Maria Fasce, mwanamke kijana kutoka katika familia nzuri, ambaye alikuwa amesoma, alijikuta akikabili hali hiyo. Alijiunga na shirika hilo kama mjumbe mnamo tarehe 6 Juni 1906, lakini akapata hali ya ukame wa kiroho katika monasteri na mnamo 1910 aliamua kuondoka kwa muda wa kutafakari lakini akarudi mwaka uliofuata. "Ninaamini alikuwa na ubadilishaji wa mambo ya ndani - kwani aliweza kujivua tamaduni zake zote, kutoka kwa kila kitu alichokuwa cha kujihusisha na masisita hawa na kuishi wakfu wake pamoja nao,” alisisitiza Bellini.
Jitihada za Mama Fasce
Kwa hivyo mnamo 1914 alichaguliwa kama Mwalimu wa Manovisi na miaka sita baadaye alichaguliwa, kwa kura ya umoja, kuwa Mkuu wa Monasteri. "Kila kitu unachokiona ukifika Cascia kinatokana na yeye, Padre Pietro alisisitiza. Mama Fasce alieneza ibada ya Mtakatifu Rita, aliendeleza mahujaji, alifanya kazi kwa bidii kujenga mahali Patakatifu panapofaa kwa ajili ya kuwakaribisha waamini, alianzisha jarida la Dalle api alle rose, yaani(Kutoka nyuki hadi mawaridi), lilitafsiriwa kwa lugha kadhaa na kuzindua mkusanyiko wa michango, ambayo ilisaidia kuunda Alveare ,yaani (Mzinga wa Nyuki), ambayo ni nyumba ya wasichana masikini. Mama Fasce aliaga dunia kunako tarehe 18 Januari 1947 na mabaki yake yaliwekwa katika Basilika ya chini ya Cascia; na kunako tarehe 12 Oktoba 1997, Mtakatifu Yohane Paulo II alimtangaza kuwa mwenyeheri. Kwa upande wa Padre Pietro, haya yote yanaonesha kwamba utakatifu unazaa, na kwamba utakatifu wa Mtakatifu Rita hunawafanya watu wengine kuwa watakatifu.”
Msamaha na Upatanisho
Na kati ya Basilika ya juu na ya chini kuna sehemu ya maungamo, mahali ambapo sakramenti ya upatanisho inaadhimishwa na ambapo kuna makuhani wa kuungamisha. Inajumuisha vyumba vitano: chumba cha mapokezi, chumba cha maandalizi, chumba cha maadhimisho, chumba cha maungamo na chumba cha shukrani. Padre Ernesto Alfonso, raia wa Angola, wa Shirika la Roho Mtakatifu, amehudumia huko kwa muda wa majuma matatu, ambaye wakati wa kuzungumza na vyombo vya habari Vatian alielezea uzoefu wake. "Katika ulimwengu ambao inasemekana hakuna mtu anayemtafuta Yesu tena, hasa katika sakramenti ya upatanisho, ambapo hapa, badala yake, tunaona kwamba watu bado wanaungama, alisema.
Mahujaji
Mahujaji wanaomba kusikilizwa, hawahitaji kusema dhambi zao tu, bali pia kuwasilisha shida zao," "kuna kilio cha msaada kwa hali nyingi," Padre Ernesto anaendelea. Tathmini yake ya saa zinazotumika katika maungamo ni kwamba kuna imani miongoni mwa watu. Wengi wanakuja Cascia ili kumshukuru Mungu kwa ishara halisi walizopokea, wengine kuomba nguvu za kukabiliana na matatizo mbalimbali, kwa hiyo, kwa kasisi wa Kutaniko la Roho Mtakatifu muujiza tayari ni ule wa kujua jinsi ya kuishi na hali nyingi maishani kwa kumtazama Yesu, ambaye ndiye nguvu zetu, njia, njia ya kufuata, ukweli na uzima. Ni, kwa vitendo, ujumbe wa Mtakatifu Rita: mtazame Yesu, samehe, upendo, tumaini, imani katikati ya giza la maisha. Hivi ndivyo watu wanatufanya tujisikie katika maungamo, anahitimisha Padre Ernesto, na kwa sisi waungamaji ni utajiri: kuzungumza na ndugu wanaotuletea shuhuda hizi pia hutusaidia kukua.”