CEI,Ulinzi dhidi ya nyanyaso:ripoti zaidi,uaminifu na mazungumzo!
Na Guglielmo Gallone na Angella Rwezaula - Vatican.
Mtandao unaopanuka, kuunda, kuwa thabiti. Na hilo ni lazima lijibu changamoto inayodai sana: mnamo 2023-2024, kulikuwa na waathrika wanaodaiwa wa unyanyasaji 115, ambapo 64 walikuwa wanaume na 51 walikuwa wanawake. Katika kipindi cha miaka miwili inayozungumziwa, kulikuwa na kesi 69 za madai ya unyanyasaji, ambapo 27 zilifanywa katika parokia na wahusika wake karibu walikuwa mapadre wote (67). Hii ndiyo taswira ambayo uchunguzi wa tatu juu ya shughuli za ulinzi wa watoto na watu wazima walio katika mazingira magumu, iliyochapishwa na Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI) na kuwasilishwa tarehe 28 Mei 2025 katika Jumba la Borromeo, katika Ubalozi wa Italia unaowakilisha nchi yake mjini Vatican.
Ahadi ya Kanisa
Hata hivyo, ripoti hiyo pia ilifanya iwezekane kufuatilia dhamira ya Kanisa katika ngazi ya eneo: CEI iliongeza huduma mahali, ilitoa mafunzo kwa waendeshaji zaidi na zaidi, na kupanua mizizi yake katika eneo, hivyo kusaidia kuimarisha wazo kwamba kulinda, kuzuia na mafunzo sio wajibu wa maadili t, lakini badala yake ni mchakato wa kikanisa ambao hunajengwa pamoja kama jumuiya. Mpango huo ulizinduliwa mwaka wa 2019 na kusasishwa mara ya mwisho kila baada ya miaka miwili mnamo 2023, toleo la tatu la utafiti unaohamaishwa na huduma ya kitaifa ya ulinzi wa watoto na watu wazima walio katika mazingira magumu wa CEI huchambua shughuli za huduma za kikanda, majimbo na vituo vya kusikiliza katika kipindi cha miaka miwili 2023-2024. Mbali na takwimu iliyo hapo juu, ripoti inaakisi kwanza ushiriki mkubwa katika mpango huo, ambapo majimbo 184 (94.2% ya jumla) na zaidi ya watu 1,100 walihudhuria mikutano (kilele kilikuwa mwaka 2022 na washiriki zaidi ya elfu tatu), na ukuaji mkubwa wa dhamira ya mafunzo ambayo, zaidi ya hayo, sio tu ya mapadre na ya kidini.
Mnamo 2024, 46.7% ya marejeo ni watu wa kawaida (ikilinganishwa na 39.7% mnamo 2022) na timu za wataalam, hasa watu wa kawaida na wanawake wengi, ambao wanasaikolojia na waelimishaji wanajitokeza, wapo katika 78.3% ya huduma. Yote hii inaonekana kuimarisha sio tu ushiriki katika mikutano ya mafunzo (22,755 mwaka 2024) ambayo lengo kuu ni juu ya heshima ya utu wa watoto na mazoea mazuri katika parokia, lakini pia imani ya waathirika: mawasiliano na vituo 103 vya kusikiliza katika eneo hilo yalitoka 38 mwaka 2020 hadi 3273 katika 2023. Idadi inayohitaji kujitolea na uaminifu unaoongezeka kila mara kwa upande wa taasisi kwa angalau sababu tatu. Ya kwanza: kikundi cha umri kilichoathiriwa zaidi kati ya waathirika wanaodaiwa wa unyanyasaji ni miaka 10-14 (31.3%). Zaidi ya hayo, wengi wa wanaodaiwa kuwa wahusika wa unyanyasaji ni mapadre (44 kati ya 67) na karibu wote ni wanaume (65 kati ya 67) wenye umri wa karibu miaka hamsini. Sababu ya tatu na zaidi ni kwamba wakuu 52 kati ya 66 wa Vituo vya Usikilizaji hawajui malalamiko yoyote ya madai.
Umuhimu wa mahusiano
Kwa hivyo, tunahitaji kuelimisha, kuongeza ufahamu, na kuegemea kwa wale wanaohitaji. Mkutano katika Jumba la Borromeo ulifanyika juu ya maswala haya. Baada ya salamu za kitaasisi za Balozi Francesco Di Nitto, Paolo Rizzi na Barbara Barabaschi wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Piacenza waliwasilisha huduma tendaji, waendeshaji waliohusika, na mipango elfu tatu ya mafunzo iliyofanywa kwa miaka miwili tu. Neno kuu, kwa kila mtu, lilikuwa "uhusiano." Kwa sababu hapo ndipo utunzaji huzaliwa, hapo ndipo kujitenga na ulimwengu wa nje kunavunjika. Hili lilisisitizwa wakati wa meza ya duara iliyosimamiwa na Ignazio Ingrao na Askofu Giuseppe Baturi, katibu mkuu wa CEI, ambaye kulingana naye: "Kanisa ni ukweli ulioenea zaidi nchini Italia na lazima tuendelee kufanya sehemu yetu ili kila mtu aweze kufikiria kufanya sehemu yake: kusaidia majimbo madogo na dhaifu zaidi, kuimarisha vituo vya kusikiliza kwa kuanzisha uhusiano wa kuaminiana, kukuza hali halisi pia katika ngazi mahalia na kitamaduni, kwa mfano na vyuo vikuu. Kujua, hata hivyo, kwamba dawa ya kwanza ya kiutamaduni ni Injili. Hii inajenga uaminifu, umoja na kwa ajili yetu, kama Papa Francisko alivyotufundisha, ina maana ya kuchukua tatizo kwa uzito" ili kuelimisha wajibu na kufanya Kanisa kuzidi kuwa nyumba salama".
Kujitolea kwa vijana: "Msiogope"
Ujumbe unaoendana zaidi na wito uliotolewa kwa vijana na Papa Leo XIV wa "wasiogope", ulisisitizwa na Askofu Giuseppe Baturi katika mahojiano na vyombo vya habari vya Vaticani: “Kwanza kabisa, kwa upande wetu ina maana ya kutoogopa kushughulikia suala hilo hata katika wigo wake wa uhalifu kuthibitisha ukweli, kuthibitisha ukweli, kuwaadhibu wenye hatia, kuunda haki, kuponya majeraha na kufahamu mizizi ya kina ya tabia dhidi ya Injili. Kutokuwa na hofu kwetu sisi Kanisa kunamaanisha kushughulikia suala hilo, tukijua kwamba ni suala la kuaminika na kwamba itatufanya kuwa mahali pa huruma ya kweli.”
Umuhimu wa Kanisa lililo wazi
Kwa mujibu wake Askofu Baturli aliongeza akisema kuwa "Lazima tufanye hata zaidi eneo la kitaifa limefunikwa, lakini kitovu cha hatua ni kati ya majimbo. Tunapaswa kuunda vituo vingine vya kusikiliza karibu na maisha ya kawaida ya watu. Hii ina maana kwamba ulinzi wa watoto wadogo unalingana na uchungaji wa kawaida: ina maana kwamba unafanyika huko, ambapo watu wanaishi". Aliungwa mkono na Monsinyo Luis Manuel Alí Herrera, wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto: "Vipengele vya kusukuma kwa namna fulani vinaonekana kwangu kuwa hivi: mfano wa kimaeneo wa ngazi nyingi, harambee kati ya dayosisi na hali halisi ya kitaasisi ya mtaa na kitaifa; mafunzo kama kichocheo cha mabadiliko ya kitamaduni; ushirikiano kati ya mwelekeo wa kikanisa na mwelekeo wa kiraia, yaani, ushirikiano na mashirika ya umma kwa jina la muungano, kanisa la uwazi".
Mafunzo na kuzuia
Monsinyo Herrera alihitimisha hotuba yake kwa mambo mawili yanayolenga kuelewa kama uwazi wa kweli unakuzwa katika ngazi ya kikanisa na jumuiya na kama mchakato wa kiutamaduni wa kuaminiana na kukaribiana kwa Kanisa na waathiriwa unahimizwa. "Njia ya miaka hii mitano imekuwa muhimu, ikiwa hatua tatu za kwanza zilikuwa za ufahamu, mbili za mwisho zilikuwa zile za ruzuku na uendeshaji. Hili lazima lipigiwe mstari. Vituo vya kusikiliza vya eneo vinazidi kuwa na uhusiano na taasisi za kiraia lakini lazima pia viwe watu wa kuwasimamia kwa muda na ambao wataanzisha nao uhusiano wenye matunda, wenye matunda kwa kila mtu, alieleza Chiara Griffini, rais wa Huduma ya Kitaifa. Hii inatuwezesha kuwasilisha matendo mema kama kielelezo leo, si tu katika suala la kusikiliza bali pia vitendo, kinga na ajira. Tumejipanga. Barabara imeshawekwa lami. Miaka hii mitano imekuwa mtihani. Sasa ni lazima kubadili mwelekeo na kufanya ulinzi kudumu ndani ya utume wa Kanisa.”
Uratibu kwa mwendelezo
Hatimaye, katika jopo la mwisho, Padre Francesco Airoldi, chansela wa Jimbo la Bergamo, Anna Deodato, aliyewekwa wakfu na mwalimu, na Padre Antonio Rizzolo, wa matoleo ya Mtakatifu Paolo, waliwasilisha ruzuku mbili mpya "Mazoea mazuri" na "Malezi ya maisha ya wakfu." Takwimmu bora iliyojitokeza pia ilitoa umuhimu kwa simulizi hili: ukuaji wa vituo vya kusikiliza, mitandao ya kikanda inayozidi kushirikiana, aina mbalimbali za mbinu zilizojaribiwa na majimbo. Lakini changamoto inabaki kuwa ya uratibu na mwendelezo. Kulinda, kusikiliza, kujali: si kauli mbiu, bali mielekeo madhubuti, iliyofuatiliwa na Papa Francisko hadi kwa wawakilishi wa huduma na wale wanaohusika na vituo vya kusikiliza katika mkutano wao wa kwanza wa kitaifa ambapo uchunguzi wa pili uliwasilishwa kwa papa mwenyewe. Na leo, katika ukumbi wa ubalozi, katika roho kamili ya mwendelezo kati ya Papa Francisko na Papa Leo XIV, uharaka na matumaini ya kufanya jumbe hizi kuishi katika kila parokia, katika kila wilaya, katika kila uhusiano ilionekana!