杏MAP导航

Tafuta

Nembo ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Barani Ulaya(CCEE) Nembo ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Barani Ulaya(CCEE) 

Ccee:Mkutano wa wawakilishi wa Mabaraza ya maaskofu Ulaya utafanyika huko Praga

Kutangaza matumaini katika Ulaya leo hii ni mada ya mkutano ambao utafanyika katika mji wa Czech kuanza tarehe 3-5 Juni 2025.Katika kitovu cha takafakari ni huduma ya mawasiliano ya kikanisa katika Kanisa katika muktadha wa sasa.

Vatican News

Baraza la Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya (CCEE) linarejea Praga, baada ya kuwa huko Februari 2023 kwa Mkutano wa Bara wa Sinodi.Linafanya hivyo kwa mkutano wa maafisa wa vyombo vya habari kutoka Ulaya yote uliopangwa kufanyika tarehe 3-5 Juni 2025, kwa ushirikiano na Baraza la Maaskofu wa Czech. Katika Mwaka huu wa Jubilei ya Matumaini, wakuu wa mawasiliano wa Mabaraza ya maaskofu wa mataifa yote ya bara la Ulaya watafanya Mkutano wao wa 35 wenye mada inayosema: “Kuwasilisha matumaini katika Ulaya ya leo.” Leo kuliko wakati mwingine wowote, Ulaya inahitaji kufanya mawasiliano yake ya Habari Njema ya hilo "tumaini lisilokatisha tamaa," katika wakati wa kihistoria ambao unahatarisha kuwa na alama ya kukata tamaa kutokana na vita vya umwagaji damu na vurugu zisizo za kibinadamu zinazoenea katika sehemu nyingi za dunia.

Mitindo ya mawasiliano ya Papa Francisko na Papa Leo XIV

Mwangwi wa sauti ya Hayati Baba Mtakatifu Francisko, pamoja na maombi ya amani ya Papa mpya Leo XIV, yanapiga mdundo wa mawasiliano yenye upatanisho na madhubuti ya mtindo wa Kiinjili wa Yesu. "Mitindo yao ya mawasiliano ina nini cha kusema kwa mwandishi wa habari wa leo? Ndiyo maswali ya waandaaji wanajiuliza: Na kwa njia hiyo "Katika muktadha wa kihistoria wa karne zote, wawasilianaji wa kikanisa wanaweza kurudia pamoja na mtunga-zaburi: "Sauti zao zaenea katika duniani nzima na miisho ya dunia imesikiliza ujumbe wao" (Zab 18: 5)," wanabainisha.

Mpango wa mkutano huo

Daniel Arasa, Mkuu wa Kitivo cha Mawasiliano ya Kitaasisi cha Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu huko Roma,(Santa Croce) atazungumza kuhusu muktadha wa siku ya leo kwa kutoa ripoti ya utangulizi yenye mada:"Huduma ya Wawasiliani wa Kanisa kwa Kanisa katika mazingira ya sasa". Wakati mada "Mawasiliano kutoka kwa Papa Francisko kwa Papa Leo LXIV” itaendelezwa na Alessandro Gisotti, naibu mkurugenzi wa wahariri wa Baeaza la Kipapa la Mawasiliano. Kikao cha mwisho kitashughulikia mada: "Mwandishi wa habari na mawasiliano ya Vatican" ambapo wazungumzaji wawili watapishana: Javier Martínez Brocal Ogáyar, mwandishi wa gazeti la kila siku la Hispania la ABC na Josef Pazderka, mhariri mkuu wa ?eský rozhlas Plus, radio ya serikali ya Czech. Programu ya mkutano huo ikiwa imetajirishwa na shughuli mbalimbali za kitamaduni za dhamana, itajumuisha pia Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Wenceslas katika Kanisa Kuu la Prague, inayoongozwa na Monsinyo Josef Nuzík, Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Olomouc na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Czech.

30 Mei 2025, 12:56