杏MAP导航

Tafuta

2025.05.26 Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Benin walifanya mkutano wao mkuu 21-23 Mei 2025. 2025.05.26 Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Benin walifanya mkutano wao mkuu 21-23 Mei 2025.  

Benin: Wasiwasi wa Maaskofu kufuatia na mashambulizi ya kigaidi kwa raia na wanajeshi

Mashambulizi ya umwagaji damu wa kijihadi kwa miezi mitatu umeongeza wasiwasi wa watu; mshikamano wa Maaskofu kwa wanajeshi waliouawa.Haya yamethibishwa katika mkutano wa Maaskofu nchini Benin ulioanza 21 hadi 23 Mei 2025.

Na Angella Rwezaula  - Vatican.

Maaskofu nchini Benin wameelezea huruma yao kwa kina ndani ya taifa zima na familia za raia wenzao waliofariki wakati wa kutimiza majukumu yao. Ni kutoka katika taarifa yao ya mwisho ya Mkutano wa 75 kipindi cha mwaka cha Baraza la Maaskofu wa Benin ambao ulifanyika tarehe 21 hadi 23 Mei 2025. Maaskofu hao walipenda kutoa heshima kwa wanajeshi 54 waliokufa katika mashabulizi mawili yaliyopangwa na kikundi cha kijihadi tarehe 17 Aprili 2025 huko Kaskazini mwa Nchi. "Kwa kufahamu sadaka zilizotolewa kwa ajili ya kulinda amani na usalama katika nchi yetu, tunawaombea mapumziko ya milele mashujaa hawa."

Kuendeleza utume dhidi ya ugaidi kaskazini mwa Benin

Maaskofu pia walikumbusha jinsi ambavyo wanaendelea na utume wao dhidhi ya ugaidi kaskazini mwa Benin: "Tuombe hata kwa ajili ya kaka zetu na dada katika mapambano ambao wako kwenye mapingano ili Bwana awe ngao yao na mlinzi wao." Mashambulizi ya tarehe 17 Aprili, yalikuwa ya umwagaji damu zaidi wakati kikundi cha kijihadi katika nchi mnamo 20219, kilitangaza watu wa Benin. Takriban wanajihadi mia moja wa Kundi la Kuunga Mkono Uislamu na Waislamu (JNIM), wakiwa kwenye pikipiki, kwa wakati mmoja walishambulia vituo viwili vya jeshi, kimoja kiko kwenye "Triple Point" - eneo ambalo mipaka ya Benin, Niger na Burkina Faso inakutana, nyingine karibu na maporomoko ya maji ya Koudou, si mbali na mji wa Banikoara. Mnamo Januari 8, shambulio karibu na Karimama, katika eneo hilo hilo, liligharimu maisha ya wanajeshi thelathini.

Makundi ya kijihadi

Eneo hilo la mpakani mara tatu limekuwa eneo lisilo salama kutokana na kuwepo kwa makundi ya wanajihadi mara kwa mara yanafanya biashara na walanguzi wa mafuta yaliyoibwa katika nchi jirani ya Nigeria. Kwa upande wa Benin, eneo hilo ni sehemu ya mbuga ya asili ya Pendjari, mojawapo ya maeneo matano yaliyohifadhiwa nchini. Uwepo wa vikundi vya wanajihadi sasa unaweka hatarini kuhifadhi bayoanuwai ya eneo hilo, pia kutishia utalii, jambo muhimu kwa uchumi wa ndani. Kama sehemu ya Operesheni Mirador, jeshi la Benin limeweka karibu wanajeshi 3,000 kwenye mpaka wa kaskazini, ambapo vizuizi vya ulinzi vimewekwa kwa matumizi ya ndege zisizo na rubani na picha za satelaiti kuzuia uvamizi wa wanajihadi, wakati bajeti ya ulinzi imeongezwa kwa 50%. Lakini hii haitoshi kuzuia vitendo vya vikundi vya kijihadi vilivyopo mashariki mwa Burkina Faso, nchi ambayo mamlaka ya Benin inajitahidi kuratibu ili kukabiliana na tishio la pamoja.

30 Mei 2025, 14:56