Ujumbe wa CEI kwa Mei Mosi:mshikamano mpya wa kijamii unahitajika!
Vatican News
Katika ujumbe wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Italia (CEI) katika fursa ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kwa mwaka 2025 ifanyikayo kila ifikapo Mei Mosi, wanaatoa wito mkubwa kuhusu “uwajibikaji kwa sababu wanasema kuwa bado kuna kazi maskini, ubaguzi dhidi ya wanawake, unyonyaji wa wahamiaji, ajali kazini na kutokuwa na usawa, yaani, kutoelewana kati ya usambazaji na mahitaji ambayo huathiri vijana. Soko ni sisi: wakati sisi ni wafanyabiashara na wafanyakazi, na tunapokuza na kuishi matumizi muhimu.”
Kazi ni matumaini
Katika ujumbe wao uonaoongozwa na kauli mbiu: “Kazi, Muungano wa kijamii unaozalishwa matumaini, ”Maaskofu wanasisitiza kwamba "mkono usioonekana wa soko hautoshi kutatua matatizo makubwa yaliyo kwenye meza leo. Ni mkono wetu unaoonekana ambao unapaswa kukamilisha kazi ya kuunda jamii ya haki na inayounga mkono na kuendelea kupanda matumaini.” Baraza la Maaskofu wakimkumbuka Hati ya Papa Francisko kwa ajili ya kutangaza Jubilei ya 2025, Spes non confundit, yaani Matumaini hayakatishi tamaa wanakumbusha kwamba “Ulinzi na kujitolea kwa uundaji wa kazi huru, ya ubunifu, shirikishi na ya kuunga mkono, ni moja ya ishara dhahiri za matumaini.”
Njia mpya za kufanya kazi
Uzoefu wa janga hili, kwa mujibu wa Baraza la Maaskofu wanasema umewawapatia njia ya kufanya kazi ambayo inawezekana kuchanganya kazi ya kibinafsi na ya mbali katika hali nyingi, na kuongeza uwezo wetu wa kupatanisha maisha ya kazi na maisha ya uhusiano, haswa katika kile kinachojulikana kama kufanya kazi kwa busara, lakini pia kuhatarisha uhusiano wa kibinadamu kati ya wafanyakazi na uhusiano wenyewe wa kifamilia.
Mgogoro wa idadi ya watu
Kwa upande wa Maaskofu, athari ya kimuundo na ya kimsingi inaoneshwa na shida kubwa ya idadi ya watu, ambayo “kwa miaka ijayo tutaona kizazi kisichobadilika kikitoka kwenye soko la ajira, kikibadilishwa hatua kwa hatua na idadi inayopungua ya vijana. Wakati huo huo, kitu cha kushangaza kinatokea, yaani, unyonyaji wa ndugu wahamiaji, na kusahau kwamba uwepo wao unaweza kuunda sababu ya matumaini kwa uchumi wetu, lakini ikiwa wataunganishwa kulingana na vigezo vya haki tu.”
Mashindano ya kimataifa
Baraza la Maaskofu wa Italia wanasisitiza kuwa “Kinachosalia nyuma ni sheria ya nguvu ya uvutano ya ushindani wa kimataifa, ambapo makampuni hutafuta kupata mahali ambapo gharama ni ya chini zaidi. Na hii inachochea kushuka kwa gharama na heshima ya kazi.”
Kazi duni
Katika ujumbe huo aidha maaskofu wa Italia wanasisitiza kuwa “Ingawa kupungua kwa kasi kwa takwimu za ukosefu wa ajira kunaweza kusababisha matumaini, tunajua badala yake kwamba nyuma ya watu walioajiriwa kuna kazi duni. Ni muhimu kuzingatia hali ya wanawake, ambao katika baadhi ya maeneo wanaadhibiwa si tu kwa malipo ya chini, lakini pia kwa ukosefu wa dhamana wakati wa ujauzito na uzazi.”
Usalama kazini
Baraza la Maaskofu Italia (CEI),wanabainisha kuwa “Hatimaye, hakutakuwa na haki kamili bila usalama kazini, ukosefu wake ambao bado husababisha waathitika wengi. Ili kutoa matumaini, tunahitaji kubadili mwelekeo huu: itakuwa mojawapo ya ishara muhimu zaidi za Jubilei pia kwa kutumia rasilimali zilizopo katika aina za ustawi na bima kwa uangalifu kwa afya na dharura za familia. Ishara nyingine ya matumaini ni kuundwa kwa uhusiano mwema kati ya waajiri na wafanyakazi, ambapo mazungumzo, utambuzi, na taratibu za ushiriki hukuza uaminifu na ushirikiano, kuweka motisha ya ndani zaidi ya mtu na kuongeza nguvu ya kampuni na ubora wa kazi.”