Mapadre 145 walitekwa nyara nchini Nigeria kati ya 2015 na 2025
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika siku za hivi karibuni zaidi utekaji nyara umekuwa tasnia inayokua inayohusiana na hali mbaya ya kiuchumi ya nchi. Huu iuanongezea ule wa tangu mwaka 2009, wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haramu ambao wamehusika na utekaji nyara mwingi, hasa kaskazini mashariki na kaskazini magharibi mwa Nigeria, pamoja na utekaji nyara mkubwa wa watoto wa shule. Na zaidi hasa utekaji nyara kwa ajili ya fidia ulienea mwaka wa 2011, ukienea katika majimbo yote 36 na mji mkuu, Abuja, hasa tangu janga la Uviko-19; wa Julai 2022 na Juni 2023, watu 3,620 walitekwa nyara katika visa 582 vya utekaji nyara, na takriban naira bilioni 5 (takriban dola milioni 3.88) zililipwa kama fidia. Pamoja na wafanyabiashara, na kwa ujumla wale wanaochukuliwa kuwa wafanyakazi wa Kanisa walio na hali nzuri wamekuwa wakilengwa zaidi.
Jimbo la Kaduna likiibuka kuwa jimbo kuu la Nigeria kwa mapadre
Ripoti ya Shirika la Kimisionari la Fides linaonesha kwamba jambo hilo ni kali sana katika Majimbo fulani, kama vile Owerri, Onitsha, na Kaduna, huku Owerri ikirekodi idadi kubwa zaidi ya kesi 47. Licha ya idadi kubwa ya utekaji nyara, mapadre wengi waliotekwa nyara waliachiliwa, ama kupitia shughuli za uokoaji za polisi au malipo ya fidia. Jimbo la Kaduna liliibuka kuwa eneo baya zaidi, huku mpadre 24 wakitekwa nyara na saba kuuawa. Idadi hii kubwa ya vifo inaonesha kuwapo kwa shughuli za kigaidi, ghasia za waasi, na kuongezeka kwa mivutano ya kidini, na kuifanya kuwa eneo hatari zaidi kwa mapadre. Maeneo mengine ya Nigeria yenye idadi kubwa zaidi ya vifo ni pamoja na Abuja, huku mapadre wawili wakiuawa, ikifuatiwa na Benin ambapo Padre mmoja aliuawa, na Onitsha, ambapo Padre mmoja pia aliuawa. Ripoti hiyo pia inaorodhesha majimbo ya Nigeria ambako mapadre waliotekwa nyara bado hawajapatikana. Majimbo hayao ni pamoja na Kaduna, Benin na Owerri.
Kesi ndogo zilizoripotiwa Lagos, Ibadan na Calabar
Kinyume chake, majimbo ya Lagos, Ibadan, na Calabar yameripoti visa vidogo, huku mapadre wote waliotekwa nyara katika maeneo haya wakiachiliwa kwa usalama. Lagos, hasa, imesalia kuwa salama zaidi, labda kutokana na hatua kali za usalama na wanamgambo.
RECOWA: mwenendo usiokubalika
Katika taarifa iliyotolewa Juma lililopotia na kunukuliwa na shirika la Kanisa Hitaji( ACI) Afrika, Baraza la Maaskofu wa Kanda ya Afrika Magharibi (RECOWA) limelaani vikali ghasia zinazofanywa dhidi ya mapadre wa Kikatoliki katika eneo zima, kuwa ni uovu ambao unazidi kushika kasi, na kubainisha kuwa mwelekeo huo haukubaliki. Wakirejea hasa Nigeria, maaskofu hao walibainisha kuwa hakuna mwezi unaopita bila habari za kutekwa nyara kwa Padre au mtawa na wakataka maombi ya kuachiliwa kwao mara moja. Pia wamewataka mapadre wanaohudumu katika maeneo hatarishi kuendelea kujitolea katika utume wao wa kuwahudumia maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii licha ya hatari zinazowakabili.