杏MAP导航

Tafuta

2025.03.11 Sanda. 2025.03.11 Sanda. 

Maonyesho ya Sanda,Roma,kioo cha Injili

Katika Basilika ya kijubilei ya Mtakatifu Yohane wa Fiorentini yamewekwa maonyesho ambayo huambatana na kutafakari kupitia ujuzi wa masalio maarufu na acheropita (Picha takatifu, inayoaminika kuwa ya kweli na yenye asili ya kimiujiza )yaani,ambayo haikufanywa kwa mikono ya binadamu.Kardinali Reina:Kuonekana kwa Mtu wa Huzuni kunatukumbusha kwamba imani haitegemei"mtu mwenye nguvu"bali juu ya mtu aliyefedheheshwa na kuuawa ambaye alishinda kifo.

Na Maria Milvia Morciano - Vatican.

Sanda ni nini? Watoto wengine walijibu swali hili kwa uwazi wao wa akili, kwa uwazi, kwa njia rahisi kuwa ni: "Ni selfie, flash."  Watoto wadogo mara nyingi hufika, kwa undani zaidi na kwa haraka zaidi, kwa hitimisho ambazo mara nyingi ni ngumu na za kutisha kwa sisi watu wazima.Mnamo tarehe 10 Machi 2025, katika Basilika ya kijubilei ya Mtakatifu Yonae wa  Fiorentini, maonyesho ya kusafiri yenye mada: "Nani Mwanaume wa Sanda" yalizinduliwa. Kardinali Baldassarre Reina, Makamu wa Papa Jimbo kuu la Roma, alieleza matumaini yake kwamba wale wanaokaribia maonesho haya watafika katika taaluma ya  kanuni  kamili ya imani. Kwa kupitia Mlango Mtakatifu hadi kwa Mtakatifu Petro, tunajihisi tumetambulishwa kwa neema ya maisha mapya." Maonyesho hayo yanajumuisha, picha, kazi za sanaa na nakala za kifalsafa za vyombo vilivyotumika katika Mateso ya Kristo, pamoja na nakala kamili ya Sanda.

Nguvu ya Msalaba

Kardinali Reina kisha alisisitiza kwamba "sote tunaona ugumu mkubwa katika kuendeleza mang'amuzi ya imani. Wengi, wakati mwingine kwa sababu tofauti, kama vile majaribu makubwa ya magonjwa, kufiwa na mengineyo, wanajitenga na imani katika Kristo Yesu." Kumwona mtu wa huzuni ambaye alijua mateso vizuri inamaanisha "kurudi kiukweli kwa Yeye ambaye uso wake ulikuwa umeharibika kiasi cha kuwa sababu ya aibu"; Yeye mwenyewe “ndiye hazina ya imani yetu.” Imani ambayo haijaunganishwa na "mtu mwenye nguvu kutoka katika mtazamo wa kibinadamu, ambaye aliwekwa kwenye kiti cha enzi cha dhahabu, ambaye alijithibitisha mwenyewe kwa nguvu ya maneno: imani yetu inazaliwa kutoka katika msalaba, kutoka kwa mtu aliyedhalilishwa, aliyetemewa mate, aliyevikwa taji la miiba, aliyeachwa peke yake, hatimaye kuwekwa kwenye mti, sababu ya aibu, akazikwa na kisha matokeo ya mwisho ya ufufuko." Turudi kwenye mada hii ya mateso, maumivu, ya shauku, kama Paulo alivyosema, akiwaandikia Wakorintho, “wengine wanatafuta hekima, wengine wanatafuta utukufu, sisi tunatafuta nguvu ya msalaba. Nini chanzo cha aibu kwa wengine, ni chanzo cha hekima kwetu, chanzo cha nguvu."

Utafiti na ukweli

Baada ya salamu za Profesa Padre José Enrique Oyarzún, mkuu wa shirika la Kipapa la Athenaeum Regina Apostolorum, ulifika wakati wa ripoti za Profesa Emanuela Marinelli, mhadhiri mgeni katika Taasisi ya Juu ya Sayansi ya Kidini (Apra) na mtaalamu wa Sanda sidonologist - mwandishi wa vitabu zaidi ya ishirini juu ya somo hilo na Profesa Rafael Pascual, mkurugenzi wa Kikundi cha Utafiti cha "Othonia" na profesa kamili katika Kitivo cha Falsafa. Walifuatilia tena sifa za ajabu za masalio ya thamani ya Torino na wakaweka katikati ya mjadala ni upi mjadala wa muda mrefu zaidi, ukweli wa Sanda.

Picha ya Sanda ni "selfie"

Profesa Emanuela Marinelli, pia mwandishi wa kitabu kilichochapishwa hivi karibuni, Contemplating the Shroud- kutafakari Sanda, kilichoandikwa pamoja na Mtaalimungu, Padre Domenico Repice, alitoa muhtasari wa mambo muhimu ya fumbo hili kuu kwenye viunga vya Vatican News- Radio Vatican. Picha pekee ambayo hakika ni acheropita ni Sanda ya Turin. Kiukweli, profesa huyo asema, “hakuna mwanasayansi ambaye ameweza kueleza jinsi mwili wa Yesu ulivyotokeza. Kuna madoa ya damu, lakini hii ni kawaida kwa maiti iliyoteswa ambayo ilikuwa na majeraha na damu ikitoka, ambayo kwa hivyo ilichafua karatasi; Ni kama aina ya selfie, alisema mtoto mmoja. Ni flash."

Nakala ya Sanda
Nakala ya Sanda

“Leo wanasayansi katika Enea la Frascati hutuambia kwamba inaweza kufafanuliwa tu kwa kukiri kwamba mwili wa Yesu, kwa wakati fulani, ulitoa mionzi ya ultraviolet. Na hilo hutuleta kwenye kizingiti cha fumbo la ufufuo. Hakuna mwingine aliye na fumbo hili na kuvutia kwa Sanda. Wale wengine wanaoitwa acheropite ni picha takatifu, bila shaka, ambapo ibada nyingi hufanywa na wale waliozifanya na wale walioziheshimu. Lakini ni kazi za wanadamu: kiukweli ni tamaduni. Mara nyingi hunakiliwa kutoka katika Sanda, kama vile Uso Mtakatifu wa Lucca au Uso Mtakatifu wa wa Kaburi Takatifu. Inashangaza kwamba msalaba unaitwa Uso Mtakatifu; Hili ni jambo la kushangaza, lakini katika karne za kwanza Sanda hiyo iliwekwa ikiwa imekunjwa ili kuonesha uso tu ambao ulinakiliwa. Juu ya Sanda inaonekana kwamba Yesu ana macho wazi, makubwa sana; baadaye tu, hasi ya picha ilituonesha kuwa kope zilifungwa. Uso Mtakatifu wa Lucca, ulioanzia karne ya 8, huzaa macho yale yale, pua ndefu, mdomo mdogo na hufunika Sanda kikamilifu. Emanuela Marinelli alisebainisha kuwa kikweli masalio ya Toscana ni nakala iliyorudiwa kwa uaminifu ya kitani kitakatifu na, kwa tafsiri, pia kinaitwa acheropita".

Mtawanyiko wa Sanda katika Sanaa na Mandilioni

Pia kuna kazi nyingine za sanaa, hasa picha za kuchora, ambazo zinathibitisha utamaduni huu wa kina na kujitolea kwa Sanda. Miongoni mwa haya, anayeitwa Mandylion ya Edessa, "uso ambao kuna mikunjo ambayo wanasayansi wa Marekani wamegundua kuwa sawa kwenye Sanda. "Msururu huu wa mikunjo" - alifafanua Profesa Marinelli - "kuthibitisha kile ambacho mwanahistoria Ian Wilson alikuwa amethibitisha: Sanda ilikuwa imekunjwa ili kuacha uso tu kuonekana. Tunaamini kwamba mandylioni ni, kiukweli, Sanda ambayo utamaduni wa Veronica ulizaliwa, picha ya kweli, Uso wa kweli. Mandylioni baadaye ilinakiliwa mara nyingi, kama ile ya Genova, pia ya zamani sana, ambayo inatoka Constantinople. Kuna tamaduni nzima ya picha ambayo ilizaliwa hasa kutoka katika uchunguzi wa Sanda."

Vidokezo ambavyo vinakuwa ushahidi

Kuna maelezo mengi yasiyoweza kukanushwa, ya nguo ya kitani, ambacho katika vyanzo huitwa kitani cha kitani, kitambaa kizuri kilichotengenezwa kwa muundo wa herringbone ambacho ni watu matajiri tu wangeweza kumudu. Mtu aliyesulubishwa ambaye haishii kwenye kaburi la kawaida, lakini hata amefungwa kwa kitani kizuri kama hiyo anaweza kuwa Yesu tu katika karne tatu za kwanza, uso wa Yesu hauoneshwi isipokuwa kwa njia ya mfano: kijana, mchungaji mwema.  Kuanzia karne ya 4 na kuendelea, habari zilianza kuenea kwamba uso wa Yesu ulikuwa na sifa ya kutamka chini ya jicho, macho makubwa, pua ndefu, nywele ndefu na ndevu. Hizi ndizo sifa za Sanda ambazo - msomi anafafanua - tunazopata katika picha zote za picha,  na taswira za Yesu."

Injili katika Picha

Ishara za Kalvari na kifo cha Kristo zimechorwa kwenye kitani kitakatifu. Hicho ni cha kifalsafa kwa sababu kusulubiwa hakuweza kufanyika katika kiganja cha mikono kwa sababu za kimwili. Huu ni usulubisho wa kweli wa Warumi wa karne ya 1 kwa sababu misumari ilipigiliwa kwenye vifundo vya mkono ili kutegemeza mwili kwani, wakati wa Yesu, sehemu za miguu hazikutumika. Sehemu ya miguu, ambayo wasanii walionesha basi, ilizaliwa katika nusu ya pili ya karne ya 1, wakati kusulubiwa kulifanyika kwenye circus na uchungu ulipaswa kupunguzwa ili kuweka maonesho; na kisha wanaingiza kipengele hiki chini ya miguu. Badala yake, Sanda inatuonesha miguu ya Yesu iliyoinama mbele sana, kwa sababu ilipigiliwa misumari moja kwa moja msalabani. Ili kuunga mkono mwili kulikuwa na misumari  kwenye mikono tu, hasa ambapo wangeweza kuunga mkono mwili.

Misumari
Misumari

Kuna athari nyingine: kwa mfano, kwenye shavu la kulia kuna ishara ya pigo kutokana na fimbo. Na tunajua kwamba Yesu alipokea pigo hili ambalo, katika Injili, linaitwa kofi kwa Kilatini, lakini kwa Kigiriki linaitwa ρ?πισμα (rapisma), yaani, aina ya pigo ambalo Yesu anapokea na ambalo lilivimbisha shavu lake lote na kuponda pua yake. Sanda ina kila kitu ambacho Injili inatuambia na zaidi: hairekodi ni viboko vingapi alipokea, wakati Sanda inatuambia kwamba alipata 120. Na kuna maelezo kwa hili: Pilato alitaka kumwokoa, kwa hivyo hakumhukumu kwa uvumi wa kawaida, lakini kwa sauti nzito ambayo, hata hivyo, ilishindwa kuufanya umati huo kuwa na huruma. Kwa hiyo liwali wa Yudea naye akajiruhusu kushawishiwa kumsulubisha. Sanda inatuletea hukumu hii maradufu.

Sanda ni habari ya picha kutoka Kalvari

Mtaalamu wa Vatican Orazio Petrosillo, mwandishi mwenza na Emanuela Marinelli wa kitabu chake cha kwanza kilichotolewa kuhusu Sanda, alifafanua Sanda kama "habari za picha" kutoka Kalvari, ufafanuzi wa wanahabari, ambao unaakisi jinsi gani mtu lazima akubali ushahidi wa kile anachokiona. Sanda pia ni ya thamani dhidi ya jaribio lolote la kusambaratisha Injili. "Huwezi kutoroka na Sanda," alisisitiza mtaalamu wa Sanda Emanuela Marinelli.

Aina ya zana zilizotumika kumpiga Yesu
Aina ya zana zilizotumika kumpiga Yesu

Jeraha la ubavu

"Mtaalimungu  anabishana kwamba jeraha la ubavuni ni la mfano, kwamba lilianzishwa ili kutoa maana ya sakramenti, damu ya Ekaristi na maji ya ubatizo, kwa hivyo uvumbuzi wa Yohane au hata wa jumuiya huleta kuzaliwa kwa Kanisa kutoka ubavu wa Kristo. Lakini juu ya Sanda hiyo kuna jeraha ambalo damu iliyoganda na serum ilitoka, kama vile Yohane asemavyo anapoandika: 'Yeye aliyeona anashuhudia kwamba ni kweli, naye anajua kwamba anasema kweli, ili nanyi pia mpate kuamini.' Kwa nini mwinjili anasisitiza? Ilikuwa ni ajabu kwamba damu na mgando wa damu(serum) zilitoka kwa mtu aliyekufa, lakini Yesu alikuwa amepiga kelele wakati wa kifo, hivyo alikuwa amekufa kwa mshtuko wa moyo.

miiba
miiba

Leo wataalamu wa magonjwa ya moyo wanatuambia kwamba tayari alikuwa ameanza kuteseka huko Gethsemane, ambako alitokwa na jasho la damu na katika dakika hiyo ya mwisho, baada ya mateso yote, alilia. Kilio cha kupasuka kwa moyo, mafuriko ya pericardium, kutenganishwa kwa sehemu nzito ya damu kutoka katika (serum ni aina ya  kioevu chenye rangi ya kahawia na chenye protini nyingi ambacho hutengana wakati damu inaganda), msukumo wa mkuki. Mfuko huu wa damu na serum hufungua na kwanza damu hutoka, kisha serum inatolewa. Sanda inathibitisha Injili kwa ajili yetu na wale wote ambao wamejaribu kuivunja Sanda hawajafaulu."

Mashtaka ya uwongo yaliangukia kwenye masikio ya viziwi

Carbon 14,  maarufu, ambayo amezungumzwa tangu 1988, alikuwa amefuatilia historia ya enzi za kati. Takwimu hii imekataliwa kabisa: sampuli ilichukuliwa kutoka kona ambayo ilikuwa imebadilishwa, kurekebishwa. Kwa hivyo kutoka  upande wa takwimu imeoneshwa: takwimu ya msingi ya uchambuzi huo ambayo ilikuwa siri katika Jumba la Makumbusho la Uingereza, kurasa 700, zilipatikana kwa mtafiti Tristan Casabianca, kutoka Corsica, takwimu msingi, ambayo wakati huo ilisomwa na Benedetto Torrisi wa Chuo Kikuu cha Catania, profesa wa takwimu ambaye pamoja na mshirika wake Giuseppe Pernagallo walionesha kuwa katika sampuli hiyo ndogo ya sentimita tatu kulikuwa na pengo la miaka 150. "Ni muda mrefu sana kuwa mwakilishi wa shuka lenye urefu wa mita 4.41.

Sanamu inayoonesha mlalo wa Yesu katika sanda
Sanamu inayoonesha mlalo wa Yesu katika sanda

Kwa hivyo takwimu hiyo ilikataliwa. Sanda imenyanyaswa, imeshutumiwa kuwa ya uwongo,” alibainisha Marinelli. Kisha profesa huyo alinukuu tena maneno ya mtoto ambaye wakati wa katekisimu, kuhusu ufufuko, alisema: "Yesu alikuwa mkali kwa wanafunzi wa Emau. Alifanya mzaha, alitoweka. Mara tu walipomtambua, alitoweka na mtoto mwingine akajibu kwamba hakuelewa chochote "kwa sababu hakupotea lakini aliteleza na kuingia kwenye mkate." Yesu anatoweka wakati anamega mkate ili kuwafanya Mitume waelewe kwamba sasa yuko pale ambapo lazima tumtafute. "Aliteleza ndani ya mkate, kwa maana kwamba lazima tumtafute ndani ya Ostia."

Kikundi cha damu

Aina ya damu ya chembe chembe za damu kwenye Sanda ni AB. Jambo la ajabu ni kwamba hata katika miujiza ya Ekaristi iliyosomwa kisayansi, siku zote ilitokana na kundi lile lile, ambalo ni la nadra zaidi: 5% ya watu wanayo na hii ni muhimu sana. Ni ya aina moja ya damu kama miujiza huko Buenos Aires na Poland. Utafiti wa kisayansi hutuleta karibu na imani. Ilionekana kuwa kinyume chake ni kweli, lakini badala yake uchunguzi wa hivi karibuni na wa hali ya juu wa kisayansi unazidi kuungana katika kuthibitisha ukweli wa Sanda. Petro na Yohane wanapoingia kaburini, Yohane alisema kwamba ile sanda iliyokuwa juu ya kichwa chake ilikuwa pale pia, imekunjwa upande mmoja. Hiki ni kitambaa kidogo zaidi sasa huko Oviedo, Hispania, kilichotiwa damu ya kundi moja la AB na Sanda. Hata poleni(pollini) nyingi zinapatana. Leso iliyokuwa imekunjwa mara mbili inaingiliana kikamilifu na Uso, lakini hakuna picha, kuna damu tu. Leso hiyo  ilitumika wakati Yesu alipokuwa bado msalabani, ambayo walimfunika nayo mara tu alipokufa na kisha kumshusha; kitambaa kilijaa damu zote zile zikimtoka mdomoni na puani.

Ugunduzi wa hivi karibuni

"Sanda ni ishara kwa nyakati zetu. Ugunduzi wa Sanda, ugunduzi halisi, ulikuja na ujio wa upigaji picha. Katika picha hasi ya picha tunaona mwili mzima vizuri zaidi kuliko kwenye Sanda yenyewe kwa sababu iliacha alama yake mbaya kwenye Sanda. Kwa hiyo kwa kupiga picha hasi na camera ya classic ikarudi katika chanya na hapa wanasayansi walipaswa kukubali kwamba hii ilikuwa kitu kisichoeleweka. Na bado haiwezi kuelezeka, ikiwa hatukubali, kama wanasayansi wa ENEA ya Frascati, kwamba picha hiyo iliundwa na mwanga mkali sana. Lakini hapa sayansi inasimama kwa sababu maiti hatoi mwanga. Na hapa pia kuna  mtoto alisema: 'Lakini huyo alikuwa Yesu, hakuwa na matatizo! Tayari huko Tabor kila kitu kilikuwa kikiangaza.' Mtoto hakutaja Tabor, alisema kwamba Yesu alikuwa amesafiri kwenda milimani pikinik pamoja na marafiki na juu ya mlima kila kitu kikawa angavu. ‘Halafu alipofufuka akafanya hivyo hivyo, akawa anang’aa na kupiga selfie na Sanda na kutuachia!’ Mtoto alitatua tatizo hilo.”

Njia ya matumaini pia pamoja na Sanda

Tunapitia kipindi kigumu ambacho, pamoja na kila kitu kingine, watu wengi wako tayari kuamini mambo ya ajabu, habari za uwongo za upuuzi zaidi. Lakini kwa nini ni vigumu kumtambua Mungu? "Kuna mkanganyiko," alijibu Emanuele Marinelli. "Kuna watu wasioamini kuwa kuna Mungu wanaoamini juu ya nyota, kwa sababu ni lazima uamini katika jambo fulani. Kuna mwandishi mmoja alisema: 'Unapoacha kumwamini Mungu, unaamini katika kila kitu kingine.' Ukweli ni hivyo, kwa sababu hata Margherita Hack, mtaalam wa nyota asiyeamini Mungu, aliwahi kusema kuwa badala ya kuamini wachawi, ni bora kumwamini Mungu.  Pia kuna ujinga, hata kwa watu waliosoma. Wengi wanasema wana mashaka lakini ukweli ni wajinga. Inahitajika kujiandikisha mwenyewe, kusoma. Watu wengi wanabaki na utamaduni wa kidini katika ngazi ya katekisimu. Ni muhimu kusonga mbele katika utamaduni wa kidini na pia katika utamaduni wa jumla: lazima usome, usome, usome kwa kina, nenda.” Ukitaka kuishi lazima utembee.

Maonyesho ya Sanda
Maonyesho ya Sanda

Maisha ni safari. Mwaka huu sisi ni mahujaji wa matumaini. Tunapaswa kutembea. Sanda ni leo kwa wana  wa Mtakatifu Thomas. Hapa, njoo, tazama, weka kidole chako, njoo na utembelee maonyesho haya katika Basilika ya Mtakatifu  Yohane Mbatizaji wa Fiorentini. Tuko karibu na Basilika ya Mtakatifu Petro, tuko kwenye njia ya mahujaji katika basilika ya Jubilei na kuna maonyesho makubwa ya Sanda. Njia ambayo, kupitia vidirisha vyote na kazi za kisanii zinazooneshwa, hutuongoza kwenye kutafakari. Kardinali Roberto Repole, Askofu Mkuu wa Torino, alitangaza kwamba mwaka huu  2025 hakutakuwa na kuweka wazi Sanda. Lakini sisi wasomi wa Sanda tumefanya kitu, tumevumbua maonyesho yaliyoenea katika makanisa yote yanayotaka. Tunaleta nakala ya Sanda na kuionyesha. Ni nakala, si ya asili, bali hata mbele ya nakala mtu anaweza kusali, kutafakari, kufikia kutimiza Jubilei takatifu na  Kwaresima takatifu. Kwanza kabisa, kipindi cha matumaini kwa sababu tunakihitaji."

13 Machi 2025, 11:08