Maaskofu wa Ulaya katika sala kwa ajili ya amani ya Ukraine na Nchi Takatifu
Vatican News
Kuanzia Jumatano ya Majivu tarehe 5 Machi 2025 na kwa kipindi chote cha Kwaresima, Kanisa Barani Ulaya linabaki kukusanyika katika 'Meza ya Ekaristi' ili kuomba amani. Mkutaniko huo unaohusisha wajumbe wote wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya(CCEE,) ni kwa kuhusisha kuandaa na kuadhimisha angalau Misa moja ya kuwaombea wahanga wa vita na kuomba kutoka kwa Bwana "amani ya haki na ya kudumu, hasa kwa ajili ya Ukraine na Nchi Takatifu."
Ishara ya matumaini kwa Ulaya
Tukio hili limepewa mada: “Mnyororo wa Ekaristi” ambalo linalenga kuwa uzoefu wa umoja na ishara inayoonekana ya matumaini kwa Bara zima la Ulaya; kwa wakati wa maombi, kufunga na kutoa sadaka kwa kujisikia kama sisi sote ni ndugu na kumwomba Mungu kukomesha vita."
Kuomba kwa ajili ya Papa
Katika siku hizi za mateso na magonjwa, aidha walitoa wito mpya kwa waamini wote kuombea afya ya Papa Francisko.