杏MAP导航

Tafuta

Kardinali Pierbattiasta Pizzaballa Kardinali Pierbattiasta Pizzaballa  (? LPJ)

Kwaresima,Pizzaballa:Msamaha una nguvu zaidi kuliko maneno ya jeuri ya chuki

Katika Ujumbe wake kwa ajili ya mwanzo wa Kipindi cha toba,Patriaki wa Yerusalemu wa Kilatini alikazia kusema,“hotuba kuu za migogoro na kashfa”hazimzuii Mungu kutamka pamoja na Yesu neno la upatanisho.Katika ujumbe wa video,Msimamizi wa Nchi Takatifu,Padre Patton,anakumbusha sadaka ya Ijumaa Kuu:"Ni msaada unaotusaidia kulinda maeneo matakatifu."

Na Angella Rwezaula – Vatican.


Moyo wa Pasaka ni Msalaba: tumaini la Kanisa na la ulimwengu limejengwa juu yake. Tumaini ambalo halikatishi tamaa, ingawa historia ya wanadamu inaonekana kutawaliwa na vita, jeuri, ubinafsi, kutoelewana. Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, Kardinali Pierbattista Pizzaballa, alirudia hayo kwa nguvu katika Ujumbe wake wa Kwaresima, na siyo kwa waamini wa jimbo lake tu lakini pia ni muhimu kwa kila mwamini kuelewa katika wakati huu wa giza na usio na uhakika, kwamba “maneno ya jeuri ya chuki na usemi wenye jeuri ya migogoro na kashfa, hayawezi kumzuia Mungu kutamka katika Kristo neno la upatanisho: "Ave Crux, spes unica!" Kwaresima inawakilisha uwezekano mpya wa zawadi iliyofanywa upya ambayo, kupitia jangwa inayopatikana pamoja na Yesu, linaongoza kwenye neema na msamaha. "Tunahitaji neno hili jipya, neno hili la Msalaba, ambalo linaweza kuonekana kuwa upumbavu kwa wenye nguvu na wenye busara wa ulimwengu huu na wa siku hizi, lakini ambalo, kwa usahihi kwa kuvuruga vigezo vya kidunia, ndilo neno pekee linaloweza kufungua tena njia za matumaini na amani," anaandika Kardinali Pizzaballa.

Kardinali aidha alizingatia maana ya njia ya Msalaba, “Via Crucis” ambayo kwayo alisema tunajifunza, kwa shida lakini kwa furaha, mantiki mpya ya kutoa na msamaha, ambayo inahitaji wanaume na wanawake, vijana kwa wazee, familia na watoto walio tayari kuifuata kwa kufanya upya fikra na mitazamo. Ni kwa njia hiyo tu tunaweza kutumaini mustakabali wa amani." Na amani inakuja kwa njia ya upatanisho ambayo inakuwa sakramenti kwa sababu Mungu ametupatanisha na yeye mwenyewe kwa njia ya Kristo. Hata hivyo, Kardinali anabanisha "neno la upatanisho, ili liwe na matokeo, lazima liwe huduma, yaani, huduma, ahadi za watu binafsi na jumuiya. Zawadi hiyo si ya kiinimacho bali inaomba kukaribishwa, kushuhudiwa, kuishi na kushirikishwa. Basi sote tujisikie kuwa tunahusika na kuwajibika pamoja, wachungaji na walei wanaume na wanawake waaminifu, watawa, katika kuleta neno na huduma ya upatanisho kwa ulimwengu: “Kwa maana tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa kazi yetu”(2Kor 5:20).

Padre Patton: "Chuki imeleta kifo na uharibifu"

Katika ujumbe wake kwa njia ya video kwa ajili ya Sadaka ya kimapokeo wa kuunga mkono huduma kwa Watu wa Nchi Takatifu itakayofanyika Ijumaa Kuu ijayo, Padre Francesco Patton, Msimamizi wa Nchi Takatifu, pia alirejea kwa uwazi maumivu hayo, akisisitiza kwamba: vita, kwa pande kadhaa, si tu kwamba vilileta kifo na uharibifu lakini vimepanda chuki zaidi kati ya mataifa jirani na ndugu. Familia nyingi ziliachwa bila kazi na kuhangaika kuwapeleka watoto shuleni pamoja na kulipia huduma za matibabu kwa wapendwa wao. Wanandoa wengi vijana wamelazimika kuahirisha ndoto yao ya kuanzisha familia na kuleta watoto ulimwenguni." Mgogoro ambao hata haujaizuia Msimamizi mwenyewe, hadi ikalazimika kuhangaikia kulipa mishahara ya walimu na washiriki wa ndani wanaosaidia katika maeneo ya mahali patakatifu na katika kazi mbalimbali za kijamii, na pia kukabiliana na gharama ya maisha ambayo imeongezeka hasa kwa sababu ya migogoro.

Msitusahahu

Padre Patton ametoa shukrani kwa Maongozi ya Mungu ambayo yamejidhihirisha kupitia mshikamano wa Wakristo kutoka duniani kote, tumeweza kukabiliana na ahadi nyingi za kiuchumi: upendo  na taasisi." Na kisha alizindua wito kwa watu wote wenye mapenzi mema kuwa: "Siku ya Ijumaa Kuu, wakati kutoa sadaka kwa ajili ya Nchi Takatifu  itakayofanyika katika  majimbo na parokia zenu, tukumbukeni na tuwe wakarimu. Wahimize mapadre wenu wa parokia wasitusahau sisi ambao, kwa mamlaka ya Kanisa la Ulimwengu wote, tunatunza mahali  patakatifu yaani  Nchi Takatifu na Wakristo wanaoishi karibu na madhabahu Takatifu  hizo.”

 

06 Machi 2025, 09:15