杏MAP导航

Tafuta

2025.03.05 IPatriaki  Sako na Askofu Msaidizi wa Baghdad, Warduni, Pamoja na Maimamu watatu wa Kiislam 2025.03.05 IPatriaki Sako na Askofu Msaidizi wa Baghdad, Warduni, Pamoja na Maimamu watatu wa Kiislam  

Iraq,Kardinali Sako:Ramadhani na Kwaresima huimarisha umoja wa kitaifa

Kwa mwaka 2025,mwezi wa Kiislamu wa kufunga unakwenda sambamba na Mafungo ya Kikristo ambapo ni ishara ya matumaini.Hii ilioneshwa na Patriaki wa Baghdad wa Wakaldayo,katika ujumbe wake kwa Waislamu na waamini wa Kikristo uliotolewa katika siku za hivi karibuni."Undugu wa kibinadamu sio wazo tu,lakini ni njia ambayo imetuelimisha na ambayo tunaishi katika maisha yetu ya kila siku."

Vatican News


Patriaki wa Baghdad wa Wakaldayo, Kardinali Raphaël Louis Sako, ametoa wito mkubwa wa matumaini katika ujumbe wake kwa waamini wa Kiislamu na Wakristo kwamba “Kutambua na uthamini nguvu mpya ya kufunga, hata kama eneo la Mashariki ya Kati na ulimwengu linaharibiwa na vita na ugaidi. Ni katika muktadha wa matukio mawili ambayo kwa mwaka 2025 yanakwenda sambamba yaani, Mfungo wa Mwezi Ramadhani wa Kiislamu na Kipindi cha Kwaresima kwa Wakristo. "Kwa ndugu zetu, ninatoa salamu zangu za kheri za dhati kwa Waislamu katika mwezi huu wa mfungo na kwa Wakristo mwanzoni mwa Mfungo wa Kwaresima, nikiomba kwamba Mwenyezi Mungu atujalie sote rehema na aijalie usalama nchi yetu tuipendayo na nchi za eneo hili. Ramadhani na Kwaresima ni nyakati za kufunga, sala, toba na msamaha, utakaso kutokana na maovu, sadaka na upendo na maadili juu ya kuishi katika roho ya upendo na uvumilivu,"alisisitiza Kardinali Sako.

Kuhimiza waamini maadili ya kidini

Patriaki wa Baghdad ya Wakaldayo hata hivyo anaomboleza: "kutengwa kwa watu wengi kutoka kwa Mungu, Mungu wa upendo na huruma lakini pia kutengwa kutoka kwa kila mmoja, kwa uvumilivu, na kwa kutenda mema. Katika kipindi cha mfungo waamini wanahitaji nuru ya Mungu kuangazia akili na mioyo yao ili kutafsiri mapenzi yake katika maisha ya wema.” Kardinali Sako alitazama kwa umakini nchi yake Iraq kwamba: “Kwa ajili ya utulivu wa kudumu wa nchi, hakuna suluhisho lingine zaidi ya kujisalimisha chini ya mantiki ya Serikali, kushirikiana nayo ili kuimarisha haki, utawala wa sheria na umoja wa kitaifa, na kutumia dhana ya uraia na si ubaguzi wa kidini. Njia ya kufikia lengo hili ni kupitia elimu na vyombo vya habari." Kwa upande wake, Kardinali Sali alibainisha kuwa: "mapadre anaitwa kuwahimiza waamini wake kwa maadili ya kidini na ya kimaadili, ili kufunga ambalo ni chaguo la moyo na roho na kugeuzwa kuwa hatua ya uongofu na wakati wa baraka kwa nchi na watu, na si kubaki tu mazoezi rasmi."Kardinali huyo alisisitiza mara kadhaa jinsi inavyofaa kwa dini mbili kuelewana kwa undani zaidi.

Msimamo mzuri wa Uislamu na Ukristo

Hata hivyo kwa hakika, katika utangulizi wa kitabu kitakachochapishwa kwa ajili ya Uislamu, Kardinali anaandika kwamba: "Haikubaliki kwamba hatujifunzi ukweli kuhusu dini ya Kiislamu na kwamba Waislamu hawajifunzi ukweli kuhusu dini ya Kikristo na dini nyinginezo, kusoma vyanzo vya kuaminika na vilivyoidhinishwa na sio kuegemea imani na chuki za watu wengi." Katika maandishi hayo, Patriaki wa Baghdad anatumaini maono mapya ambayo yanafungua njia ya uhusiano bora wa ushirikiano, mbali na mwelekeo wa kutawala na itikadi kali. “Ni wakati wa kutakasa mioyo yetu na kujirekebisha katika nuru ya ukweli, kwa sababu imani ni jambo moja na udini ni jambo lingine." Kwa upande wa Kardinali, kuna tofauti kati ya Uislamu wa kidini na wa kisiasa. “Uislamu wa kweli unakubali kuishi pamoja na kwa watu wote bila kuwa na utofauti.

Udugu wa kibinadamu sio wazo tu bali ni njia ya maisha yetu ya kila siku

 

Ukristo ni njia ya upendo iliyooneshwa na Kristo ambaye aliwaalika wanafunzi wake kuishi kama watoto na ndugu zake wao kwa wao, kwa upendo na amani. Udugu wa kibinadamu si wazo tu, bali ni njia ambayo imetuelimisha na ambayo tunauwakilisha katika maisha yetu ya kila siku. Katika Uislamu kuna wito wa rehema, ambao Waislamu wengi wanafanya bila kuzingatia utambulisho wa watu. Upendo na huruma havitenganishwi, rehema inawakilishwa katika upendo,” anaadika katika kitabu hicho. Hatimaye, Kardinali anasisitiza kwamba “ni lazima tuthibitishe kwa ujasiri na uwazi yale tuliyo nayo pamoja na kutambua kwa uaminifu yaliyo tofauti, kuanzia na dhana kwamba Mungu alituumba tofauti ili tuweze kupenda na kushirikiana. Hivi ndivyo Mungu anataka, ambaye anaenea kwa upendo wake wote na rehema" alihitimisha Patriaki Sako.

06 Machi 2025, 09:47