杏MAP导航

Tafuta

2025.03.12 Askofu Christian Carlassare wa Jimbo la Bentiu, Sudan Kusini. 2025.03.12 Askofu Christian Carlassare wa Jimbo la Bentiu, Sudan Kusini. 

Askofu Carlassare:Sudan Kusini inaendelea kusahaulika na kunyonywa

Katika taifa la Afrika,mapigano kati ya wanajeshi wa kawaida na wanamgambo hayakomi.Askofu wa Bentiu,Christian Carlassare, anatoa wito wa amani,kazi na mazungumzo ya kijamii,huku akilaani kuachwa kwa jumuiya ya kimataifa. "Makanisa nchini yameungana na Papa katika wakati huu wa udhaifu wa kimwili."

Na Massimiliano Menichetti

Taifa changa zaidi duniani, Sudan Kusini, liko hatarini kwa mara nyingine tena kuzama katika dimbwi la ghasia zisizo na mwisho. Kwa miezi kadhaa sasa, Vikosi vya Ulinzi vya Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF), vikiongozwa na Rais Salva Kiir, na wanamgambo wa White Army, wanaoshirikiana na Sudan (People's Liberation Movement - In Opposition (SPLA-IO), wanaohusishwa na Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar, wamekuwa wakitofautiana. Jamhuri hiyo iliyozaliwa mwaka wa 2011 baada ya miongo kadhaa ya migogoro, tayari imekumbwa na hali ya kutisha ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya 2013 na 2018, hali ambayo sasa inaonekana kujitokeza tena. Uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba 2024 umeahirishwa hadi mwishoni mwa 2026, na uwezekano wa kuharibu mikataba ya amani iliyotiwa saini mwaka wa 2018. Kwa upande wa Christian Carlassare, Askofu wa Bentiu, ni muhimu kujenga amani na kurejesha matumaini kwa idadi ya watu.

Jimbo la Bentiu,Sudan Kusini
Jimbo la Bentiu,Sudan Kusini

Pengine imesalia kuwa miongoni mwa nchi maskini zaidi kwa sababu imesahauliwa na kutelekezwa na maslahi na usaidizi wa kimataifa, wakati ni mwathirika wa mienendo ya kimataifa ya unyonyaji wa rasilimali, mafuta kwanza kabisa kwa sasa, lakini pia rasilimali nyingine. Haya yote yanachochewa na ukweli kwamba taasisi hizo bado ni masikini na hazina uwezo wa kusimama na wananchi na kudhamini utawala wa sheria

Je,  watu wanaishije hali ya sasa?

Idadi ya watu huelekea kuishi hali hiyo kwa kujiuzulu. Kiukweli, haijawahi kujua taasisi zenye uwezo wa kuhakikisha mazungumzo ya kijamii, utatuzi wa migogoro bila kutumia vurugu, na utulivu wa kiuchumi ili kukuza biashara, ili kazi izae mali na maendeleo. Mara nyingi watu huishi kwa akili zao na wale wanaotajirika hufanya hivyo kwa kuchangamkia fursa hiyo, wakati mwingine kwa njia zinazotia shaka sana. Wengi wanategemea misaada ya kibinadamu kama fursa muhimu lakini, kwa wakati huu, hata misaada hii ya kibinadamu inatiliwa shaka. Ni zoezi muhimu katika mchakato wa kuleta demokrasia ya nchi. Yapo matazamio ya Mkataba wa Amani kama kilele cha mchakato huo, kufuatia utekelezaji wa Maazimio mengine mengi. Mojawapo ya Maazimio hayo ni, kwa mfano, lile la kuungana kwa jeshi la taifa, kukomesha makundi mengi ya wanamgambo yanayowajibu viongozi au makundi mbalimbali.

Jimbo la Bentiu
Jimbo la Bentiu   (Foto: Sr. Sylvie Lum Cho, MSHR/Ghana)

Katika miaka ya nyuma kumekuwa na majaribio ya kuwaita waajiri kwa mafunzo, lakini hawajawahi kuwekwa katika mikoa yote ya Sudan Kusini, kwa nini?

Yamebakia makundi yenye silaha ambayo hayajibu kwa Wafanyakazi wa Serikali Kuu; bado kuna ukabila wa makundi haya yenye silaha: tatizo liko hapa! Na siasa inaonekana kuhusika, kwa sababu inazitumia inapowezekana, ingawa haina udhibiti kamili juu yao. Kwa sababu hivyo ndivyo hutokea kwa vurugu: mara tu unapoitumia, huna udhibiti tena juu ya kile ambacho vurugu inaweza kufanya ndani ya nchi. Siku hizi, kiukweli, tunafuatilia kwa wasiwasi hatua ya serikali kubadili kikosi kilichopo Nassir. Katika jaribio hili lilipambana na wanamgambo wa eneo hilo, wanaojulikana kama White Army, ambao ni vijana waliosajiliwa kutoka katika vikundi vya upinzani dhidi ya serikali.

Ni kitu gani kilianzisha mgongano huo?

Sababu ya mapigano haya inaonekana kuwa uwepo, pamoja na wanajeshi wa serikali, wa wanamgambo wengine wanaopingana na wa ndani mahali hapo. Kwa hiyo tunapokea habari za migongano inayotokea kutokana na fikra fupi za viongozi wasio na uwezo wa kujihusisha na mazungumzo kabla ya kufanya maamuzi. Kwa hivyo, kutokuelewana huko katika mji mkuu basi hutafsiri kuwa migongano katika maeneo, kwa sababu lugha sawa haizungumzwi na hakuna uelewa sawa wa shida ambazo wakazi wa eneo hilo hupata huko katika eneo waliko.

Maisha ya Jumuiya ya Bentiu
Maisha ya Jumuiya ya Bentiu

Turudi kwenye uchaguzi. Kwa nini kuahirishwa hadi 2026?

Tunahitaji kuelewa kama kuna nia ya kufikia uchaguzi au kama, hata katika mazingira ya kisiasa, kuna shauku  tu ya kudumisha hali ya sasa na mizani yake: na, kiukweli, mizani isiyo imara sana lakini mizani hata hivyo. Ninaamini kwamba swali kwa viongozi wetu ni jinsi gani inawezekana, leo, kuweka nchi pamoja katika hali hii ya mgogoro mkubwa wa kiuchumi, kujaribu kutodumisha makundi sawa ya kisiasa, au vikundi vilivyo madarakani bali kuwa na watu wenye uwezo kama wasimamizi wa nchi ambao wanaweza kukabiliana na hali mbaya zinazotokea katika ngazi zote: usalama, maendeleo ya kiuchumi, afya, elimu; ambapo Mawaziri wenye dhamana kweli wana uwezo wa kutekeleza njia itakayopelekea nchi kuwa bora kuliko ilivyo sasa.

Papa alitembelea nchi hiyo mwaka wa 2023 na kusisitiza kwa nguvu hitaji la ushiriki wa jumuiya ya kimataifa katika mchakato wa maendeleo, akinyooshea kidole silaha na unyonyaji. Je, ni urithi gani wa ziara hiyo?

Kumbukumbu ya ziara ya Baba Mtakatifu mjini Juba bado iko wazi sana kwa watu, na kwa hakika inatoa nguvu na mamlaka makubwa kwa huduma ya Kanisa katika nchi inayoitaka uinjilishaji, pamoja na mchakato wa mazungumzo na upatanisho. Utulivu unaoweza kupatikana pale tu idadi ya watu inapojipatanisha na maisha yake ya nyuma na kutambua kwamba hakuna njia nyingine zaidi ya kuishi kwa udugu kati ya makabila yote yaliyopo nchini. Kuna watu wengi wa Sudan Kusini ambao tayari wamejihusisha na njia hii - ninafikiria jumuiya ya kiraia,  lakini wengine wengi ambao bado wamevunjwa akili au kubadilishwa ili kudumisha mgawanyiko na maslahi ya baadhi ya makundi.

Watoto wa Bentiu
Watoto wa Bentiu

Jinsi gani Jumuiya zinaishi nchini kwa sasa?

Makanisa nchini Sudan Kusini yameungana kumzunguka Papa na kumwombea katika wakati huu wa udhaifu wa kimwili; na Papa anatufundisha kwamba wale wanaoonesha njia siku zote sio wenye nguvu zaidi, wenye nguvu, wenye afya njema, bali ni wale ambao ni dhaifu na mara nyingi huwekwa kando, labda hata wagonjwa kama yeye sasa, labda wana mtazamo tofauti wa ukweli. Na kwa hivyo mwaliko ni kwa wale wenye mwendo wa haraka, wa kuupunguza mwendo, kuwakaribia masikini, wa mwisho, na kujifunza aina nyingine ya mwendo, ambao sio wa haraka, wa haraka wa uchumi na masilahi ya ulimwengu wetu wa kisasa, bali ule wa udugu, ambao ndio mwendo pekee unaozalisha jumuiya na ushirika.

Haja watoto waje kwangu..
Haja watoto waje kwangu..

Je, kuna uhusiano gani kati ya imani zilizopo?

Tuna makanisa mengi ya Kikristo, au madhehebu ya Kikristo, uwepo mzuri wa Waislamu pia. Kuna heshima, lakini si mara zote ushirika. Njia ya pamoja ni ile ya imani na matumaini: maono na mtazamo wa maisha unaotuunganisha. Sasa tunapitia kipinidi cha Kwaresima wakati Waislamu wanapitia Ramadhani yao. Wote wakamgeukia Bwana. Kwa hiyo, imani hii pia inatuita kuimarisha upendo wetu wa kidugu ili kila mmoja asizingatie nyumba yake mwenyewe tu, bali katika familia ya wanadamu wote, ambapo hakuna mali ya kidunia inayoweza kugawanya au kutilia shaka umiliki wetu wa mwisho wa Mungu.

Sudan Kusini pia inakabiliwa na janga la mafuriko na joto kali ambalo linasababisha maelfu ya wakimbizi wa ndani ...

Mabadiliko ya tabianchi yanachangiwa na tabia zetu na unyonyaji wa maliasili, kwa mfano ukataji miti karibu na miji ili kutengeneza nishati ya mafuta, umefanya baadhi ya maeneo ya tambarare bila uoto wa asili na maeneo ya maisha kukosa watu pia kutokana na kuwepo kwa ubadhirifu kila mahali. Suala jingine ni usimamizi wa bonde la Mto Nile: mabwawa, usafishaji wa mto na kwa hivyo mtiririko wa maji, matuta ambayo kiukweli hayapo. Eneo la Jimbo letu, katika Jimbo la Umoja, limefunikwa na maji kwa asilimia 40 na takriban watu 800,000 wamehamishwa kwenda sehemu za juu, wakipoteza mifugo na ardhi ya kulima. Kufanya mambo kuwa magumu zaidi, pia kuna uchafuzi unaozalishwa na makampuni ya mafuta, hivyo maji - karibu na viwanda vyao - si salama lakini watu wengi hawana chaguo na huchota maji hata kama yamechafuliwa.

Hacha watoto waje kwangu:ufalme wa Mungu ni wao
Hacha watoto waje kwangu:ufalme wa Mungu ni wao

Katika hali hii inaongezwa maelfu ya wakimbizi wanaokimbia mzozo nchini Sudan...

Katika eneo hilo, pamoja na waliokimbia makazi yao, kuna takriban wakimbizi 130,000 wa Sudan ambao wanategemea misaada kutoka katika mashirika ya kibinadamu. Kwa hivyo leo tunaangalia kwa wasiwasi siasa za kimataifa za wakati huu, tukizidi kuwa na mashaka juu ya misaada. Kwa hakika kuna haja ya mageuzi katika suala la mbinu na mazoea, lakini misaada ya kibinadamu bado inasalia kuwa njia ya mwisho kwa watu wengi wanaotafuta maisha na hadhi.

Ni nini kinahitajika?

Tunahitaji muda wa utulivu wa kisiasa na kiuchumi, tunahitaji amani ili kuweza kushughulikia matatizo halisi ya nchi: kutojua kusoma na kuandika; ukosefu wa shule na walimu wenye sifa; ukosefu wa huduma ya afya ya umma ambayo inamfikia kila mtu; ya miundombinu na barabara zinazounganisha nchi; na uwezekano wa kuwekeza katika kazi na hivyo pia kuzalisha maisha kwa ajili ya jamii ambazo kweli zinaishi katika hali ya umaskini mkubwa.

Mwashamu tangu Agosti 2024, umekuwa ukiongoza Jimbo la Bentiu, eneo la takriban kilomita za mraba elfu 38 na zaidi ya wakazi milioni moja…

Sisi ni jimbo changa sana, tuliozaliwa bila miundo lakini tukiwa na jumuiya kubwa ya waamini ambao wanakusanyika kumzunguka Mungu katika sala ili kuendeleza maisha katika mazingira ya hofu, ukosefu wa usalama na kifo. Tunajenga juu ya urithi wa kazi ya makatekista wengi na waamini walei ambao wameifanya jumuiya hii kuwa ya Kikristo. Sasa ni suala la kupanda neno la Mungu kwa mikono miwili, ili maisha na matendo yawe ya kiinjili kweli. Inahusu kushiriki kwa watu imani na tumaini la mabadiliko yanayoweza kutokea, ambapo mtu halazimiki tena kuishi kulingana na mambo yanayofaa, lakini ambapo anaweza kuishi katika udugu. Tuna parokia saba zenye eneo kubwa sana, mapadre tisa wa Jimbo, na jumuiya mbili za kitawa  za Kikomboni na Wafransiskani.

Askofu Carlassare,Jimbo la Bentiu, Sudan Kusini
Askofu Carlassare,Jimbo la Bentiu, Sudan Kusini

Je, ni hatua zipi zitafuata ili kufanikisha misheni hii?

Tutaimarisha mafunzo ya mawakala wale wa  kichungaji, huduma ya haki na amani, na masomo kwa watoto wetu. Pia tutajaribu kukuza shughuli za kiuchumi, kijamii hasa zile zinazohusiana na kilimo na utunzaji wa mazingira tunamoishi. Jambo la muhimu ni kuweza kuhamasisha jumuiya za wenyeji, kama jumuiya za imani na matumaini: ambazo zinaweza kuathiri maisha ya pamoja ya jamii pana. Ili kutika katika uchumi wa fujo, dhuluma na ushindani, kwa hiyo uchumi wa vurugu, tuweze kuishi uchumi wa udugu. Kwa kutimiza kile kisemacho kuwa “Tazama jinsi wanavyopendana”: na kwa upendo huu jamii nzima inaundwa.

Unatamani nini katika mwaka huu wa Jubilei, unaoakisiwa pia na matatizo ya nchi na mivutano na vita vingi duniani?

Matashi yangu  mema kwa Jubilei na maneno ya Mika: "Umefundishwa yaliyo mema, ambayo Bwana anataka kutoka kwako: kutenda haki, kupenda kwa huruma, na kutembea kwa unyenyekevu na Mungu wako." Hapa, haya ndiyo matashi yangu kwa Kanisa la Bentiu wakati huu, kwa Sudan Kusini, na pia kwa safari hii ya pamoja ambayo ulimwengu unaitwa kuichukua, kuishi pamoja kama ndugu wakitambuana kama watoto.

13 Machi 2025, 12:23