杏MAP导航

Tafuta

Asia na Oceania kwa pamoja wamefanya kozi kwa kwanza ya kurugenzi za kitaifa za Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa(PMS). Asia na Oceania kwa pamoja wamefanya kozi kwa kwanza ya kurugenzi za kitaifa za Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa(PMS).   (?bogdanserban - stock.adobe.com)

20-23 Februari ilifanyika Kozi ya kwanza ya Kurugenzi ya PMS ya Asia na Oceania huko Sydney!

Kuanzia tarehe 20 hadi 23 Februari ilifanyika Kozi ya PMS ya Asia na Oceanea kwa mara ya kwanza huko Sydney nchini Australia.Kwa siku hizo ilikuwa ni mwaliko wa Baba Mtakatifu wa kuwa:“Wamisionari wa Matumaini kati ya Watu,”ambayo ni kauli mbiu ya Siku ya Kimisionari Duniani ijayo.Na pia walitumia fursa ya kusali kwa ajili ya Papa Francisko ili aweze kupona na kurudi katika huduma yake.

Na Angella Rwezaula – Vatican.


Asia na Oceania pamoja kwa mara ya kwanza katika mkutano wa mabara wa kurugenzi za kitaifa za Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa (PMS). Mkutano huo uòianza tangu tarehe 22 hadi 24 Februari 2024 huko mjini Sydney nchini Australia. Wakurugenzi wa kitaifa, wanaowakilisha zaidi ya nchi 20 kutoka mabara hayo mawili, kwa kuongeza na Bangladesh, Kambodia na Laos, Indonesia, Kazakhstan, Korea, Lebanon, New Zealand, Visiwa vya Pasifiki, Pakistan, Ufilipino, Sri Lanka, Timor Leste, Vietnam na Papua New Guinea na Visiwa vya Solomon, walikazia umuhimu wa kufanya kazi pamoja juu ya uharaka na matumaini katika hali tofauti za umisionari.

Kozi iliyofanyika kwa siku zote tano ilikuwa ni mwaliko wa Baba Mtakatifu Francisko wa kuwa: “Wamisionari wa Matumaini kati ya Watu”, ambayo ni kauli mbiu ya Siku ya Kimisionari Duniani 2025. Washiriki wa mkutano huo pia walitumia fursa ya kutoa  ujumbe wa upendo wa ukaribu  na katika sala kwa ajili ya Askofu wa Roma, ambaye kwa sasa amelazwa katika hospitali ya Agostino Gemelli mjini Roma kwa sababu ya ugonjwa wa  mkamba(Bronchtis  na mengine yaliyooingezeka.

"Misheni ya Kikatoliki (jina la kurugenzi ya kitaifa ya PMS ya Australia) imekuwa na bahati ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa mabara wa Wakurugenzi wa Kitaifa wa PMS wa Asia na Oceania," alisema Padre Brian Lucas. "Australia ina uhusiano mzuri sana na majirani zetu wa karibu, ikijumuisha kusaidia ofisi ya mkoa huko Phnom Penh, na fursa hii ya mwingiliano wa kibinafsi hutoa msingi mzuri wa kufanya kazi pamoja." Kuleta pamoja nguvu bora na kutafuta isho za kukabiliana na dharura za ndani ni lengo la tukio hili ambalo, pamoja na kutoa vipindi vya mafunzo (pamoja na mada ya Jubilei "Mahujaji wa Matumaini.)

Pia alijumuisha katika mpango huo fursa kwa washiriki kukutana na baadhi ya wawakilishi wa Kanisa la Australia akiwemo Askofu Mkuu Charles Balvo, Balozi wa Kitume nchini Australia, na Vincent Long Van Nguyen OFM, Askofu wa Jimbo la Parramatta. Kwa kuongezea, Wakurugenzi wa Kitaifa wa PMS ya Asia na Oceania walikutana na wajumbe wa Sinodi, kama vile Mons. Kelly Paget, Chansela wa Jimbo la  Broken Bay. "Tunajaribu siku hizi kuungana kama kanda mbli. Bila shaka, tuna matatizo, changamoto na matumaini tofauti, na hilo ndilo tunalozungumzia. Matumaini yetu ni kuwakilisha sauti moja inayoweza kufanya kazi kwa ajili ya misheni ya Kanisa  ulimwenguni  kote kwa kuleta mabadiliko madhubuti,” alishirikisha Padre Michael Cheng Chai, Mkurugenzi wa Kitaifa wa PMS New Zealand.

 

24 Februari 2025, 11:49