Kujenga siku zijazo na kutafakari juu ya matumaini ni kichwa cha Kitabu kipya cha Kardinali Bagnasco
Na Edoardo Giribaldi – Vatican.
Katika mojawapo ya maswali yanayoongoza kitabu kipya cha Kardinali Angelo Bagnasco, kiitwacho Christ, the Hope of Every Man, “Kristo Matumaini ya kila Mwanadamu” kitachapishwa na Toleo la Ares ni “Inawezekanaje usijifungie mwenyewe kwa sasa peke yako na kupondwa na upweke?" Kitabu hiki katika wakati wa Jubilei na kinarejea tena huduma ya Kardinali, na kutualika kutazama zaidi, kuelekea upeo wa maana unaoweza kuwa msingi wa kujenga siku zijazo. Rais wa zamani wa Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI) na Shirikisho la Baraza la Mabaraza ya Maaskofu Barani Ulaya (CCEE), Kardinali Bagnasco katika kurasa hizo anatoa mawazo ya tafakari ya kila siku ili kuambatana na tafakari na sala wakati wa Mwaka Mtakatifu 2025.
Haja ya kuinua macho
Kitabu hicho kitachapishwa mnamo tarehe 3 Machi 2025 ambapo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la wa Genova, Marco Tasca anashirikisha maoni yake kwamba "Kardinali anamwongoza msomaji katika safari ya kila siku ya roho na akili ya imani, akiwa na ufahamu kwamba mwanadamu wa kisasa, licha ya ahadi na vikwazo, anahisi haja ya kuinua mtazamo wake juu. Huu ni mwaliko unaoendana na maneno ya Baba Mtakatifu Francisko, anayetuhimiza kutafuta nafasi ndogo za muda kusoma Injili kati ya ahadi moja na nyingine, ili kurejea kwetu na kukutana na Bwana, katika ulimwengu ambao Kardinali Bagnasco anausisitiza kuwa tunahitaji sana matumaini."
Uharaka wa kutangaza matumaini
Maandishi ya kardinali yanalenga hasa kuonyesha kwa busara njia za kumkaribia Mungu, na anatuhimiza tutafute tumaini la Jubilei. Mfano muhimu unapatikana katika tafakari iliyotolewa kwa siku ya Pasaka, ambayo mwandishi anaandika: "Bwana amevuka mto mkali wa kifo na kurudi kwenye ufuko wa maisha." Maneno yaliyochukuliwa kutoka kwenye mahubiri yaliyotolewa mwezi Aprili 1999, alipokuwa Askofu Mkuu wa Pesaro, jukumu ambalo yeye mwenyewe anakumbuka katika utangulizi wa kitabu kama utangulizi wa dharura: lile la "kutangaza matumaini ambayo hayatashindwa kamwe: Yesu Kristo". Na leo, katika nyakati ngumu lakini wakati huo huo wa jubile, tumaini hili ni "zaidi" muhimu zaidi kuliko hapo awali.