杏MAP导航

Tafuta

Askofu Willy Ngumbi Ngengele wa Jimbo la Goma,DRC. Askofu Willy Ngumbi Ngengele wa Jimbo la Goma,DRC. 

DRC: watu wa Goma bado wanaogopa kukosa usalama

Hali katika mji wa Goma bado haujatengamaa kutokana na kuwa mikononi mwa waasi wa M23.Shule nyingi bado zimefungwa,pia kwa sababu majengo mengi ya shule yameharibika au kuharibiwa kutokana na vita.Mahospitali hayana madawa.Alisema hayo Askofu Willy Ngumbi Ngengele wa Jimbo Katoliki la Goma nchini DRC.

Vatican News.

Mji wa Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo)ni shwari, lakini watu bado wanaogopa kuondoka majumbani mwao na kujitosa kwa sababu usalama haujahakikishwa kikamilifu. Alisema hayo Askofu Willy Ngumbi Ngengele wa Jimbo la Goma wakati akizungumza na Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari Fides kutoka Goma, mji mkuu wa Kivu Kaskazini, ambao umezidiwa na waasi wa M23. Alipoulizwa kuhusu hali ya shule, Askofu Ngumbi alisema, "Shule nyingi bado zimefungwa, pia kwa sababu majengo mengi ya shule yameharibika au kuharibiwa kutokana na vita. Hali mbaya zaidi ni katika hospitali zinazopokea majeruhi wengi. Taasisi za afya pia zinatatizika kutokana na uhaba wa dawa na vifaa.

Kadhalika alielezea kuwa muunganisho wa Intaneti unabaki kuwa mgumu; watu wanafanya masuluhisho ya muda ili kukaa na uhusiano na ulimwengu wa nje. Kabla ya kuangukia mikononi mwa waasi, Jiji la Goma tayari lilikuwa na wakimbizi wa ndani wapatao milioni moja na wengi wao wakiwasili kutoka mikoa ya kaskazini ya Goma katika maeneo ambayo kwanza yaliangukia mikononi mwa waasi. Hali yao kwa sasa haijulikani kwa sababu kambi za wakimbizi pia zimefungwa, na wale waliohamishwa ambao bado wana nyumba ambayo haijaharibiwa wanarudi kwao. Wale ambao hawawezi kurudi wanachuchumaa popote wanapoweza katika mazingira hatarishi,”Askofu wa Goma alisema.

Kusitisha mapigano kwa sababu za kibinadamu

Ni mgogoro mgumu. Kusitisha mapigano kulitangazwa na muungano wa wanamgambo wenye uhusiano wa kisiasa unaojiita Muungano wa (Alliance Fleuve Congo), ambao M23 ni mhusika muhimu. Wakitangaza kusitisha mapigano kwa upande mmoja kwa sababu za kibinadamu, waasi hao pia walipinga taarifa iliyotolewa awali na M23 kwa kusema hawana nia ya kuchukua udhibiti wa Bukavu au maeneo mengine nchini Congo. Hapo awali, M23 walisema walikuwa na nia ya kuendelea na maandamano hadi mji mkuu wa Congo, Kinshasa. Kwa sasa suluhisho linaendelea, lakini watu bado wanaogopa kujitosa nje kwa sababu hawajisikii salama kabisa," alisema Askofu Ngumbi.

Maaskofu wawasilisha mradi wao wa amani

Katika jitihada za kutatua mgogoro huo kwa amani, Rais Felix Tshisekedi alipokea ujumbe wa Maaskofu kutoka Baraza la Kitaifa la Maaskofu wa Congo (CENCO) mjini Kinshasa. Wakati wa mazungumzo hayo, Mkuu wa Nchi walikabidhiwa mpango wa upatanisho ulioanzishwa na CENCO na Kanisa la Kristo nchini Congo(ECC). Mpango wa upatanisho uliobuniwa na mashirika hayo mawili ya Kanisa ni mpango unaopendekeza mkakati wa kutoka katika mgogoro wa mashariki mwa Congo.

 

06 Februari 2025, 10:11