Congo(DR):ombi la Wajesuit la amani:kuheshimu uhuru wa nchi
Na Guglielmo Gallone na Angella Rwezaula – Vatican.
Jumuiya ya Shirika la Yesu, kupitia matamshi yake mengi, kutoka Chuo Kikuu cha Hekima hadi Huduma ya Wakimbizi ya Kijesuit, "inalaani vikali unyanyasaji unaoendelea na ukiukwaji wa haki za binadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo" kwa wito wa "kuheshimiwa kwa uadilifu na uhuru wa nchi na haki za watu waliohamishwa kurudi katika ardhi ya mababu zao." Kwa sababu, taarifa ya Wajesuit inakazia, "miongo kadhaa ya vita vya kutumia silaha vimewanyima wanaume, wanawake na watoto wengi sana mahitaji ya kimsingi kama vile chakula, huduma za afya na elimu."
Hali ya ardhini
Kusonga mbele kwa kasi kwa kundi la waasi ha Harakati ya (M23) mashariki mwa Congo kunaonekana kama kilele cha vita vya miongo kadhaa katika eneo la Kivu, ambalo sasa limegubikwa na mgogoro mkubwa wa kibinadamu na usalama. Kwa mujibu wa habari za hivi karibuni, wapiganaji wa msituni wanaoungwa mkono Rwanda wa kundi la M23 - baada ya kulishinda jeshi la Kinshasa na kuuteka mji mkuu wa jimbo la Goma huko Kivu Kaskazini mwezi Januari, sasa wameingia katika maeneo mengine ya eneo la mashariki mwa Congo, wakiingia Kanyabayonga na Bukavu wakiwa na silaha mkononi, mji mkuu wa Kivu Kusini, takriban kilomita 50 kutoka mpaka na Burundi, na kuelekea Butembo, mji wa pili kwa watu wengi zaidi katika Kivu Kaskazini na kitovu kikuu cha kibiashara cha jimbo hilo, ukikabiliwa na upinzani mdogo kutoka kwa jeshi la serikali. Ndivyo ilivyotokea Kamanyola na Luvungi. Kwa hivyo, waasi hao wamepiga hatua kuelekea Uvira, jiji la pili kwa ukubwa katika Kivu Kusini linalotazamana na Ziwa Tanganyika, ambapo barabara inaelekea Burundi, ambayo tayari imezidiwa na misururu ya watu waliokimbia makazi yao ambayo, kulingana na Umoja wa Matia (UN), haijawahi kutokea katika miaka 25 iliyopita.
Majukumu ya jumuiya ya kimataifa
Licha ya ushiriki mkubwa wa wahusika wa kikanda na mzozo wa kihistoria katika maeneo haya - ambayo yalizuka katika miaka ya 1990 lakini unatokana na tofauti za kikabila za karne nyingi-tahadhari ya kimataifa kwa mzozo huu imekuwa kidogo kihistoria. Hii inadhihirishwa na kutoweza kufanya mazungumzo na upatanisho katika Umoja wa Mataifa, ambapo Waziri wa Mambo ya Nje waCKongo, Therese Kayikwamba Wagner, wakati wa mkutano wa mwisho wa Baraza la Usalama, aliishutumu Rwanda "kutayarisha mauaji." Kwa sababu hiyo, Wajesuit, katika wito wao, walihimiza "jumuiya ya kimataifa, mashirika ya kibinadamu na serikali kuongeza msaada wao kwa jamii zilizoathirika." Kwa Jumuiya ya Kijesuit,"ni muhimu kuhamasisha misaada ya haraka ya kibinadamu ili kupunguza mateso na kuhakikisha kwamba msaada unawafikia wale wanaohitaji bila vikwazo." Umoja wa Mataifa, pamoja na mashirika ya kikanda, "lazima kuboresha mikakati ya ulinzi wa amani, kuhakikisha usalama wa watu walio hatarini wakati wa kuwezesha usaidizi wa kibinadamu. Ulinzi wa raia lazima ubaki kuwa kiini cha uingiliaji kati wa kimataifa, na hatua madhubuti za kuzuia ukatili mkubwa na kurejesha utulivu."
Mgogoro Uliosahaulika
Kuibuka tena kwa mzozo huu "uliosahaulika" kwa kweli kunatokea katika mwaka ule ule ambao ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa MONUSCO ulipaswa kumalizika baada ya miaka 25. Hii inafichua kutokuwepo kwa mkakati wa pamoja wa kutatua kukosekana kwa utulivu kwa muda mrefu katika maeneo haya, ambayo yana utajiri mkubwa wa maliasili kwani ni dhaifu na yanakabiliwa na masilahi ya nchi tatu. Na kwa mara nyingine tena, wakazi wa eneo hilo ndio wanaolipa matokeo. Mkasa wa hivi punde zaidi ulitokea jana, wakati takriban watu 22 walikufa baada ya mashua iliyokuwa imejaa mizigo kupinduka katika Ziwa Edward. Mbali na kutengwa na jamii ya Wakongo, majanga kama hayo pia yamehusisha takwimu za kitaasisi na kidiplomasia nchini DRC. Hasa miaka minne iliyopita leo, , Balozi wa Italia Luca Attanasio, aliyeuawa huko Goma ni ishara ya mazungumzo na diplomasia, lakini juu ya amani yote amani.