杏MAP导航

Tafuta

Kuondolewa kwa kambi ya wakimbizi wa ndani ya Bulengo nchini DRC Kuondolewa kwa kambi ya wakimbizi wa ndani ya Bulengo nchini DRC  (AFP or licensors)

COMECE,yapongeza EU kutoa Euro milioni 60 kwa Msaada wa kibinadamu huko DRC!

Kwa kuungana na ombi la Papa Francisko kuhusu mamlaka mahalia na Jumuiya ya Kimataifa fanya kila linalowezekana kutatua mzozo kwa njia za amani,COMECE inapongeza mgao wa hivi karibuni wa Umoja wa Ulaya wa Euro milioni 60 kwa ajili ya msaada wa kibinadamu na kuhimiza juhudi zaidi ili kuhakikisha kuwa misaada inawafikia walio hatarini zaidi.Haya yamo katika tamko la COMECE kuhusu matendo ya haraka ya Jumuiya za Umoja wa Ulaya katika Muktadha wa mgogoro DRC.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Askofu Mariano Crociata, Mwenyekiti wa Tume ya Shirikisho ya Mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa Nchi za Ulaya(COMECE),Jumatano tarehe 12 Februari 2025, amechapisha tamko huku akielezea ulazima wa matendo ya haraka ya Jumuiya za Umoja wa Ulaya katika Muktadha wa Kibinadamu, Mgogoro wa Usalama na Kisiasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Tamko hilo linaongozwa na mada: “Kiungo kimoja kikiteseka, mwili wote huumia”( Kor. 12:26 ). Rais huyo anaandika kuwa “ Kama Rais wa Tume ya Mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya (COMECE), ninataka kueleza masikitiko yangu makubwa na wasiwasi wa dharura kuhusu janga hilo hali ya Goma na maeneo ya jirani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Akiwa ameguswa sana na hali za kutisha Askofu Willy Ngumbi Ngengele M. Afr., Askofu Jimbo la Goma, hivi karibuni akiwa katika zira yake katika Sekretarieti ya COMECE alishirikisha hali halisi akiomba Umoja wa Ulaya na jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka ili kuhakikisha kukomesha uhasama pamoja na heshima kamili kwa hadhi ya binadamu na sheria za kimataifa. Mji wa Goma, kitovu muhimu cha kibinadamu, kiuchumi na usafiri mashariki mwa DRC, nchi jirani ya Rwanda, imetumbukia katika machafuko baada ya kutekwa na M23 waasi na washirika wao.

Kulingana na takwimu za hivi karibuni za Umoja wa Mataifa, karibu watu 3000 wamekufa na zaidi ya milioni moja wamekimbia makazi yao katika majuma ya hivi karibuni, na maelfu kujihifadhi katika makanisa, shule na kambi za muda huku kukiwa na uhaba wa chakula, maji na vifaa vya matibabu. Hospitali, ikiwa ni pamoja na vifaa vinavyoendeshwa na Kanisa kama vile Upendo, Hospitali kuu ya Uzazi, imelipuliwa kwa bomu, na kuwaua watoto wachanga na kuwajeruhi raia vibaya. Mashirika ya kikatoliki yanaripoti hali mbaya, na hospitali kuzidiwa na ukatili wa kijinsia umekithiri. Kwa kuungana na ombi la Papa Francisko kuhusu “mamlaka mahalia na jumuiya ya kimataifa kufanya kila linalowezekana kutatua mzozo huo kwa njia za amani”, COMECE inapongeza mgao wa hivi majuzi wa Umoja wa Ulaya wa Euro milioni 60 katika msaada wa kibinadamu na kuhimiza juhudi kubwa zaidi ili kuhakikisha kuwa misaada inawafikia walio hatarini zaidi.

Hupatikanaji wa msaada wa kibinadamu katika maeneo yenye migogoro na ulinzi wa raia, hasa wanawake hayana kikomo na watoto, kutokana na ukatili na unyonyaji wahakikishwe msaada kwa elimu, afya na makazi kupitia ushirikiano na mitandao ya kanisa mahalia, ambayo hubakia kuwa njia ya maisha kwa watu waliohamishwa, na inapaswa kuendelea. Chanzo kikuu cha mgogoro huu - miongo kadhaa ya unyonyaji wa rasilimali, kuingiliwa na wageni na vurugu za mzunguko - hutaka ujasiri wa kisiasa na mazungumzo ya kidiplomasia. Tunakaribisha wito wa "Mkataba wa Kijamii wa Amani na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Eneo la Maziwa Makuu," umoja wa Kanisa Katoliki na la Kiprotestanti kukomesha ghasia na kuhamaisha kuishi kwa amani na mshikamano wa kijamii. Huku wakihamasisha mchakato wa amani unaojumuisha ushirikishwaji wa Makanisa na mashirika ya kiraia, COMECE inahimiza EU pia kuunga mkono juhudi za upatanisho za kimataifa na kikanda, ikiwa ni pamoja na hatua za kuleta utulivu zilizokubaliwa hivi karibuni katika Mkutano wa Pamoja kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADC).

Kuhusika kwa majeshi ya kigeni na wanamgambo, hasa madai ya Rwanda kuwaunga mkono M23, ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa. Tangazo la waasi wa M23 kwamba wanapanga kuendeleza mzozo huo hadi kufikia mji mkuu na kudhibiti nchi inawakilisha changamoto kubwa kwa DRC na eneo hilo. EU na jumuiya ya kimataifa lazima iweke shinikizo kwa wahusika hawa kusitisha uungaji mkono wao kwa M23, kujadiliana kwa nia njema, kuheshimu uadilifu wa eneo na mamlaka ya DRC, kusitisha unyonyaji wa maliasili yake. Mazingatio ya kiuchumi hayapaswi kuathiri kujitolea kwa EU kwa maadili na kanuni zake kuu. Tunatoa wito kwa Bunge la Ulaya kuidhinisha wito wa kupitishwa kwa vikwazo vinavyolengwa na kutathmini upya masharti ya ushirikiano wa kiuchumi, ikiwa ni pamoja na ‘Mkataba wa Maelewano kuhusu Minyororo ya Thamani ya Malighafi Endelevu’, pamoja na wale wanaohusika na ukiukaji wa haki za binadamu na sheria za kimataifa.

Zaidi ya hayo, wakati tukilaani uporaji wa maliasili, tunatoa wito wa kuwepo kwa uwazi zaidi katika mazoea ya uchimbaji madini ambayo yanachochea migogoro, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mifumo ya uchunguzi wa kina kwenye minyororo ya ugavi inayohusishwa na madini ya Kongo (k.m. kobalti, coltan, na dhahabu). Kwa kuhitimisha tamko hilo “ Ninapenda kuwahakikishia Maaskofu wa DRC sala zetu zinazoendelea kwa ajili ya watu wanaoteseka kwa ajili ya amani ya haki na ya kudumu. COMECE itafuatilia kwa karibu hali hiyo mashinani na kubaki inapatikana ili kuwasilisha kwa taasisi za Umoja wa Ulaya wasiwasi wowote, mitazamo na mipango ya Kanisa la mahali hapo.”
 

12 Februari 2025, 15:47