Siku ya kupinga Biashara haramu ya binadamu:vijana jijini Roma na Talitha Kum!
Na Sr Bernadette Reis – Vatican.
Wanatoka Australia, Cameroon, Japan, Albania, Romania, Ukraine, Kenya, Mexico, Uruguay, Peru. Wameungana na Harakati ya Talitha Kum, mtandao wa kimataifa wa watawa wanaopambana na biashara haramu ya binadamu, kama mabalozi wa vijana. Juma lao la shughuli ya kuhamasisha jijiji Roma liilianza Jumamosi tarehe 1 Februari , wakati Dominika saa 6 Mchana waliungana na Papa Francisko katika uwanja wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya kusali sala ya Malaika wa Bwana. Kisha, Jumatatu tarehe 3 Februari mabalozi hawa wa vijana wakawa mahujaji wa matumaini, wakielekea kwenye Basilika ya Mtakatifu Petro, wakitembea kimwili lakini pia kidijitali "wakiwa na silaha" na kutumia Programu ya simu ya kutembea kwa hadhi , kwa lengo la kuwashirikisha hata wengine kila kona ya dunia ambayo ilihesabu kila hatua yao. Hatua ambazo zimevuka kizingiti cha Mlango Mtakatifu na zinazochangia katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu na zitafaidika na mipango mingi ya Harakati ya Talitha Kum iliyoenea duniani kote.
Siku ya Februari 8
Baada ya lile la Basilika ya Mtakatifu Petro, vijana hao pia walipitia Milango Mitakatifu ya Mtakatifu Yohane huko Laterano na Mtakatifu Maria Mkuu. Siku ya Alhamisi tarehe 6 Februari, watapitia Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Paulo Nje ya Kuta. Sr Abby Avelino, mratibu wa kimataifa wa Harakati ya Talitha Kum, alisema mabalozi hao vijana wamechukua fursa ya Mwaka wa Jubilei na hija ya matumaini kuwaalika watu wengi kutembea nao, kwa heshima. Wito huu ulizinduliwa hasa wakati wa Juma la shughuli zinazotangulia Siku ya kumi na moja ya Maombi na Tafakari dhidi ya Biashara Haramu ya Binadamu, ambayo itaadhimishwa Jumamosi tarehe 8 Februari 2025, sambamba na siku kuu ya Mtakatifu Bakhita mwathirika wa Biashara haramu ya Binadamu.
Milioni 50 watumwa wa kisasa
Kwa kutumia Programu ya Kutembea kwa Hadhi, mabalozi wachanga wanaweza kutangaza programu kupitia simu, kuongeza ufahamu kuhusu biashara haramu ya binadamu, na wakati huohuo kuchangia mipango iambayo watawa wameifanya, alieleza Sr Abby. "Watawa wetu wanafanya kazi katika ngazi ya chini na wanachama 6,000 wa Talitha Kum. Tunapotembea kwa heshima na watu, bado tunafahamu ni watu wangapi bado wanaishi katika hali ya utumwa mamboleo yaani milioni 50 ndio makadirio.” Kutembea pamoja, kwa hivyo, tunaweza kuota na kutumaini kukomesha biashara haramu ya binadamu." Programu ya Kutembea kwa hadhi ilizinduliwa tarehe 30 Januari 2024 na mabalozi wa vijana wa Talitha Kum. Kupitia hilo, wanawaalika wenzao kushiriki katika kuwahudumia waathiriwa wa biashara hiyo kwa kutembea pamoja. Hatua zao zinapohesabiwa na kuchangiwa, wanaweza kufungua maudhui na kujifunza jinsi Talitha Kum hutekeleza dhamira yake.