杏MAP导航

Tafuta

Huduma shufaa ni muhimu katika utunzaji wa mgonjwa wa muda mrefu. Huduma shufaa ni muhimu katika utunzaji wa mgonjwa wa muda mrefu.  (?pattilabelle - stock.adobe.com)

Baraza la Maaskofu wa Italia limechapisha Hati kuhusu mwisho wa maisha!

Baraza la Maaskofu Italia walichapisha dokezo kuhusu mwisho wa maisha ambapo linasisitiza umuhimu wa kipaumbele cha huduma na usaidizi wakati wa ugonjwa. "Utekelezaji kamili wa sheria juu ya huduma ya matibabu ndiyo matumaini ya maaskofu wa Italia.

Vatican News

Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia alichukua nafasi kwa niaba ya Baraza nzima kuandika barua iliyoidhinishwa wakati wa mkutano uliofanyika tarehe 18 Februari 2025. Katika ujumbe wake anabainisha kuwa “Kazi ya kwanza ya jumuiya ya kiraia na mfumo wa afya ni kusaidia na kuponya, si kuharakisha kifo."  Kwa niaba ya Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI), ofisi ya rais inaeleza kujali kwa mipango ya hivi karibuni ya kikanda kuhusu mada ya  mwisho wa maisha.  Idhini ya mwisho oliyokubaliwa katika siku za hivi karibuni za sheria ya kujiua kwa kusaidiwa na matibabu na Baraza la Mkoa wa Toscana nchini Italia.

Utunzaji na usaidizi kama kipaumbele

Kama ilivyorejewa na Mkutano wa Maaskofu wa Triveneto mnamo 2023, msaada na utunzaji ndio kipaumbele cha mfumo wa afya na - kunukuu kile kilichosemwa pia na maaskofu wa Emilia-Romagna mnamo 2024, "kupata kifo, moja kwa moja au kwa njia ya kujiua kwa kusaidiwa na matibabu, kunapingana sana na thamani ya mtu, kwa malengo ya serikali na taaluma yenyewe ya matibabu".

Hapana ubaguzi 

Kwa hivyo, Rais wa CEI anatualika kutolifanya suala hili kuwa sehemu ya mgawanyiko wa kisiasa na maoni ya umma, lakini badala yake tulichukulie kama fursa ya kutafakari kwa kina juu ya msingi wa dhana ya mtu mwenyewe ya maendeleo na hadhi ya mwanadamu", kama ilivyoainishwa pia na maaskofu wa Toscana mwaka huu.  Kwa ajili hiyo, Urais wa Baraza la Maaskofu unatarajia kuanza kwa “mjadala mpana wa bunge unaowakilisha nchi na mahitaji halisi ya raia wake.

Suala la huduma shufaa

Kwa hiyo tunatumaini kwamba katika mfumo wa sasa wa kisheria na udhibiti  tutafika, katika ngazi ya kitaifa, hatua zinazolinda maisha kwa njia bora zaidi, kukuza kuambatana na huduma katika ugonjwa, kusaidia familia katika hali ya mateso. Tunasisitiza, hata hivyo, kwamba sheria juu ya huduma shufaa bado haijatekelezwa kikamilifu: hizi ni lazima zihakikishwe kwa kila mtu, kwa njia yenye ufanisi na wa kufanana katika kila Mkoa, kwa sababu zinawakilisha njia madhubuti ya kupunguza mateso na kuhakikisha utu hadi mwisho, pamoja na maonesho ya juu ya upendo kwa jirani. Katika maisha hakuwezi kuwa na ubaguzi au michezo ya kubahatisha. Utu hauishii kwa ugonjwa au ufanisi unaposhindwa. Sio juu ya ukaidi, lakini juu ya kutopoteza ubinadamu.

Maoni ya CEi kwa mwisho wa maisha
20 Februari 2025, 12:30