Watoto wa Papua New Guinea watatumbuiza tamasha la dakika 5 kwa ajili ya Papa
Vatican News
Baadhi ya watoto 70 kutoka Mpango wa Malkia wa Mbingu (QOP) wameratibiwa kumwimbia Baba Mtakatifu Francisko katika ziara yake ya kitume ijayo nchini Papua New Guinea mwezi Septemba 2024. Padre Miguel de la Calle wa kikundi cha Orchestra cha QOP alisema kuwa watoto watacheza ala za muziki na kumwimbia papa mnamo tarehe 8 Septemba 2024 huko Vanimo. “Watoto wa Bendi ya Mpamgo wa Malkiwa wa Mbingu (QOP) wamefurahi sana, kwani Papa Francisko atawasikiliza ana kwa ana,” Alisema Padre huyo katika ripoti yake kwenye (The National), gazeti la ndani ya nchi hiyo. Padre Miguel alisema watoto hao watamsubiri Papa Francisko mwishoni mwa safari yake ya kilomita 13 ya gofu huko Vanimo ili kuwabariki watu.
Papa licha ya kutembelea kiti cha magurudumu,atakwenda kutembelea watu
Mwalimu Jesus Briceño, ambaye ataongoza kikundi hicho, alielezea tamasha la dakika 5 kama ni kama “dhahabu safi,” akiongeza kwamba wanatayarisha “vipande viwili vya muziki” kwa ajili ya Papa. Kardinali John Ribat, Askofu Mkuu wa Port Moresby, alielezea ziara ya Papa Francisko huko Papua New Guinea kuwa “baraka.” Askofu Mkuu alibainisha kuwa "Papa anayekuja, sio tu kama kiongozi wa Kanisa Katoliki tu lakini pia kama mkuu wa serikali. “Ningependa kusisitiza kwamba Papa anakuja kama mtu asiye na afya nzuri, na hivyo atakuwa kwenye kiti cha magurudumu. Yeye atafikisha miaka 88 mwaka huu. Katika umri wake na masuala yote yanayozunguka afya yake, bado aliamua kuja.”Alisisitiza kiongozi hiyo. Aidha Kardinali Ribat aliwakumbusha waamini kwamba: "Papa ni mtu kama ninyi na mimi." Hata hivyo, alikazia “ikiwa Yesu Kristo alimchagua afanye kazi hiyo muhimu ulimwenguni, tunahitaji kujitayarisha vyema kwa ajili ya kuja kwake na kumkaribisha.”