Ujurumani,Askofu Meire:Haki za binadamu ni pamoja na uhuru wa imani!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kesho, tarehe 22 Agosti 22024, tunaadhimisha Siku ya Kimataifa ya kukumbuka Wathiriwa wa Ukatili kwa Sababu za Dini au Imani, iliyoanzishwa na Umoja wa Mataifa manmo mwaka 2019. Tunataka kuwakumbuka watu wengi ulimwenguni wanaoteseka kwa jeuri kwa sababu ya dini au imani yao. Hayo yalisemwa na rais wa Tume ya Kikanisa Ulimwenguni ya Baraza la Maaskofu wa Ujerumani, Askofu Bertram Meier (Augsburg). Aliyasema hayo tarehe 21 Agosti 2024 katika mkesha wa siku hiyo ya kimataifa huku akionesha wasiwasi wa siku hiyo ya ukumbusho ambayo alisema “bado ni muhimu: kwamba “Kwa bahati mbaya, badala ya kupungua, tunaona ongezeko la mara kwa mara la jeuri dhidi ya watu kwa sababu ya imani yao au uhusiano wa kidini. Kwa mujibu wale alisema “Ni lazima tuangalie jinsi kutovumiliana na ubaguzi wa kidini mara kwa mara unavyosababisha mashambulizi dhidi ya wale wanaofikiri tofauti. Sifikirii tu kuhusu ndugu na dada Wakristo wanaoteseka kutokana na kutengwa na kuteswa ulimwenguni, bali pia watu wote walioathiriwa na vurugu za kidini.”
Wakristo hatuwezi kubaki na sintofahamu za mateso ya waathiriwa
Askofu Meier akiendelea alisisitiza kwamba: “kama Wakristo hatuwezi kubaki kutojali mateso ya waathiriwa. Kwa sababu mashambulizi haya daima ni mashambulizi dhidi ya utu wa watu, ambayo ni msingi wa haki za binadamu na ambayo, kwetu sisi, inategemea sura ya watu wote kama Mungu. Haki za binadamu pia zinajumuisha uhuru wa dini. "Kuwalinda ni kazi ya pamoja", kwa sababu kwanza kabisa ni jukumu la kila Taifa kudhamini uhuru wa kidini wa raia wake.”
Nchi zote duniani zina jukumu la kupambana na ukiukwaji wa haki za binadamu
Nchi zote zina jukumu la kupambana na ukiukwaji wa haki za binadamu na kwa hivyo pia uhuru wa kidini. Ambapo hili halifanyiki au Serikali yenyewe inashambulia haki hizi, ubaguzi na, hatimaye, vurugu, hasa dhidi ya dini ndogo, haziko mbali." Pili, Askofu Meier, alisisitiza kuwa dini zina wajibu zaidi: "Jumuiya za kidini na kwa hivyo sisi kama Kanisa tuna jukumu la kupinga kwa uthabiti unyanyasaji wa imani yetu na ubaguzi dhidi ya wale wa imani zingine. Kwa hivyo naweza tu kusisitiza kwa mara nyingine tena jinsi mazungumzo kati ya dini ni muhimu kwa kuishi pamoja kwa amani. Tunapoanza kuelewana na kuheshimiana, tunaweza kuondoa vyanzo vya chuki na vurugu."