杏MAP导航

Tafuta

2024.08.13 Esperanti na  Laudato Si e Laudate deum 2024 huko Arusha Tanzania. 2024.08.13 Esperanti na Laudato Si e Laudate deum 2024 huko Arusha Tanzania. 

Tanzania,Arusha:Congamano la Esperanti kimataifa,3-10 2024!

Kuanzi tarehe 3 hadi 10 Agosti 2024 lilifanyika Congamano la 109 la Esperanti Kimataifa.Ni moja ya mikutano muhimu uliofanyika huko Arusha nchini Tanzania kwa kuwaona washiriki 850 kutoka nchi 66 katika mabara yote matano.Walijikita na mada ya “Laudato si'”na“Laudate Deum,"ambazo ni Nyaraka mbili za Kitume za Papa Francisko.

Na Gloria Fontana na  Angella Rwezaula – Vatican.

Tangu tarehe 3 hadi 10 Agosti 2024, katika jiji la Arusha, nchini Tanzania, lilikuwa mwenyeji wa Kongamano la 109 la Kiesperanti Kimataifa . Hii ni mojawapo ya mikutano muhimu zaidi ya Kiesperanto iliyowaona washiriki 850 kutoka nchi 66 katika mabara yote matano. Katika Juma hilo la  mkutano programu mbalimbali za kitaalamu, kisayansi na kiutamaduni zilifanyika. Kwa ajili ya tukio hilo, mchango muhimu pia ulitolewa na Umoja wa Kimataifa wa Waesperanti wa Kikatoliki (IKUE - Internacia Katolika Unui?o Esperantista). Katika tukio la mkutano huo, kwa mujibu wa kaulimbiu ya mkutano huo: “Lugha, mtu na mazingira kwa ajili ya ulimwengu bora” Umoja wa Waesperanti wa Kikatoliki Kimataifa ulihariri tafsiri mbili muhimu katika lugha ya Kiesperanti.

Waraka wa Laudato si na Laudato Deumu

Ya kwanza ilikuwa ni Waraka wa Papa Francisko wa “Laudato Si',  kuhusu utunzaji bora wa Mazingira nyumba yetu ya pamoja, na wa pili ulihusu mwendelezo huo huo yaani Waraka wa Kitume wa Papa Franciskowa wa “Laudate Deum,” yaani Sifa Iwe kwa Mungu. Maandishi yaliyotafsiriwa ni matokeo ya ushirikiano wa karibu wafasiri kumi waliobobea wa Kiesperanti. Matoleo yote mawili yaliwasilishwa wakati wa kongamano hilo, ambalo lilibua mjadala wa kuvutia kuhusu ulinzi wa mazingira na ufahamu wa mtu binafsi kwa ajili ya kuhifadhi nyumba yetu ya pamoja. Kwa kuchangia  mada ya kongamano hilo, rais wa Umoja wa Kimataifa wa Waesperanti wa Kikatoliki Marija Belo?evi? alitoa hotuba yenye mada “Laudato si”.

Mwanzo wa Harakati ya Kiesperanti

Katika Juma la  mkutano huo, Umoja wa Waesperanti wa Kikatoliki Duniani uliwajibika kutekeleza Ibada ya Kiekumene na Misa Takatifu, iliyoadhimishwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu na Padre Mhesperanti, Gabriel Anda, wa Jimbo la Edea nchini Cameroon.  Kongamano hilo, ambalo lilifanyika kwa mara ya kwanza katika bara la Afrika, lilitoa fursa kwa Waesperanti wengi wa ndani, wakiwemo wazungumzaji wengi bora wa lugha ya kimataifa, kufanya mazungumzo na kukutana. Wengi pia walipendezwa na harakati za Waesperanti Wakatoliki. Ikumbukwe kwamba Wakatoliki wa Kiesperanti walianzisha shirika lao tayari mwanzoni mwa karne ya 20. Mara tu baada ya kuonekana kwa miongozo na kamusi za kwanza za Lazzaro Ludovico Zamenhof mnamo 1887, shauku kubwa katika lugha hii mpya ilianza katika nyanja ya kiutamaduni ya Kikatoliki.

Mwanzilishi wa Harakati ya  Waesperanti wa Kikatoliki alikuwa padre Emile Peltier, ambaye mnamo mwaka 1903 alijitolea kuchapisha jarida la kimataifa la “Espero Katolika” yaani ‘Tumaini la kikatoliki’, chombo rasmi cha IKUE, ambalo kwa sasa ni mojawapo ya majarida kongwe zaidi ya Kiesperanti katika dunia nzima. Huko Boulogne sur Mer (1905) Waesperanti wa Kikatoliki walikutana kwa mara ya kwanza na misa ya kwanza katika Kiesperanti ilifanyika. Zamenhof pia alishiriki tukio hilo. Mnamo mwaka 1909 huko Barcelona Wakatoliki waliandaa makongamano mbalimbali na huko iliamuliwa kufanya kongamano la kwanza la Waesperanti wa Kikatoliki huko Paris, Ufaransa mnamo tarehe 1 Aprili 1910 ulizaliwa Umoja wa Kimataifa wa Waesperanti wa Kikatoliki. Mwaka 1990, Hati ya Baraza la Kipapa la Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa pamoja na kanuni za kuadhimisha Misa na kitabu kinachohusika katika lugha ya kimataifa, liliruhusu kuchapishwa kwa Kitabu cha Misa ya Kiesperanti. Tarehe 11 Februari 1992, Umoja wa Kimataifa wa Waesperanti wa Kikatoliki, kwa Barua ya Baraza la Kipapa la Walei, la wakati ule ulitambuliwa kama chama cha Waamini Waesperanti.

Karama ya Harakati hii:Timiza Agizo la Yesu.Enendeni ulimwenguni

Karama ya Umoja wa Wakatoliki wa Kimataifa wa Esperanti ni: kwa njia ya Kiesperant timiza agizo la Yesu Kristo: “Enendeni ulimwenguni kote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe” (Mk. 16:15); ili kuonesha umoja wa Kanisa kwa kutumia lugha ya kimataifa katika liturujia na matendo yake ya kitume; kuchangia kuundwa kwa maelewano kati ya wanadamu, udugu na amani katika ulimwengu wa leo na kufuatilia ili “wote wawe kitu kimoja” (Yh17:21). Utayarishaji wa uhariri na habari: Jarida la Muungano wa Kimataifa wa Waesperanti wa Kikatoliki, “Espero Katolika” na matangazo ya Radio Vatican kwa Waesperanti, wanasambaza elimu ya Kanisa na kutumika kama njia ya habari kwa Waesperanti wa Kikatoliki.

Katika miaka minne iliyopita, Muungano wa Kimataifa wa Waesperanti wa Kikatoliki pia umekuwa ukifanya kazi kwa bidii katika uwanja wa mtandaoni. Kongamano na makongamano hupangwa na - kile ambacho ni cha kipekee zaidi kuliko nadra - sala ya kawaida ya rozari hufanyika kila siku ambayo hufurahia ushiriki wa Waesperanti kutoka sehemu mbalimbali za dunia: kutoka Brazil, Cuba, Marekani kupitia nchi za Ulaya hadi Korea na Ufilipino. Matendo ya hisani yanazidi kuwa makali zaidi. Kwa hakika, msaada wa mara kwa mara kwa parokia ya Kamerun (Mouanko, Jimbo la  Edea), ambapo Umoja wa Kimataifa wa Waesperanti wa Kikatoliki umeweka paneli za jua, ilizindua mradi wa ufugaji wa samaki na kuanzisha shule ya watoto. Watakatifu watetezi wa Waesperanti wa Kikatoliki ni: Mama Yetu wa Matumaini, Mtakatifu Pio X, Mtakatifu Maximilian Kolbe, Mtakatifu Yohane Paulo II na Mtakatifu Titus Brandsma.

Kongamanola Waespiranti Kimataifa huko Arusha Tanzania
13 Agosti 2024, 11:30