杏MAP导航

Tafuta

2024.05.08 Askofu Mkuu Raphael Thattil - wa Kanisa la Syro Malabar 2024.05.08 Askofu Mkuu Raphael Thattil - wa Kanisa la Syro Malabar 

Qatar:tabia ya kimisionari ya Kanisa la siro-malabar kuthibisha miaka 25

Kanisa la siro-malabar iliadhimisha miaka 25 tangu kuanza liturujia yake huko Doha.Maadhimisho yalianza kwa Misa Takatifu iliyoadhimishwa na Kardinali Mar George Alencherry na kufuatiwa na semina kuhusu 'tabia ya kimisionari ya Kanisa la Syro-Malabar'ambayo iliendeshwa na Dk.Kochrani Joseph,msemaji wa Kanisa la Syro-Malabar.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumuiya ya Kikatoliki ya Qatar iliadhimisha Jubilei ya mwaka mmoja kwa miaka 25 ya Kanisa la Syro-Malabar la Mtakatifu Thomas wa Doha kwa shughuli za kiutamaduni na kidini. Mnamo tarehe 3 Julai 2024, katika tukio la sikukuu ya Mtakatifu Thomas, tukio la kipekee huko Doha, maandamano ya masalio ya Mtakatifu yalifanyika katika jumba la kidini, kutoka katika  Kanisa la Kilatini la Mama yetu wa Rozari hadi Kanisa la Syro-Malabar. Hivi karibuni pia sherehe ilifanyika katika Mlima Mtakatifu Thomas, makao makuu ya Kanisa la Syro-Malabar huko Kakkanad (Cochin, Kerala), katika kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 ya Misa Takatifu ya kwanza katika Liturujia ya Syro-Malabar iliyoadhimishwa huko Doha.

Kanisa la Syro Malabar

Aliyezindua maadhimisho na mkutano huo alikuwa Askofu Aldo Berardi, O.SS.T, Vicariate wa Kitume ya Kaskazini mwa Arabia, inayojumuisha Qatar, Bahrain, Kuwait  pamoja na Saudi Arabia. Askofu Berardi alisisitiza umoja wa jumuiya na utume wake wa kutolea ushuhuda wa imani. Na kwa upande wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Syro-Malabar, Mar Raphael Thattil, aliyehudhuria hafla hiyo, alielezea matumaini yake ya kutimizwa kwa ndoto ya muda mrefu ya Kanisa iliyoongozwa na yeye kuanzisha muundo wa kikanisa huru katika eneo la Ghuba. Maadhimisho hayo yalianza kwa Misa Takatifu iliyoadhimishwa na Kardinali Mar George Alencherry na kufuatiwa na semina kuhusu 'tabia ya kimisionari ya Kanisa la Syro-Malabar' ambayo iliendeshwa na Dk. Kochrani Joseph, msemaji wa Kanisa la Syro-Malabar. Kisha kikao kilifanyika ambapo wengi walishiriki uzoefu wao. Askofu Mkuu amewashukuru na kuwaenzi kwa utambulisho maalum zaidi ya wafanyakazi sitini wa zamani waliorejea baada ya kuhudumu nchini Qatar katika miaka ya kwanza ya uwepo wa Kanisa la Syro-Malabar. Wanaosimamia sherehe za Jubilei ni, miongoni mwa wengine, Kasisi Nirmal Vezhaparampil, OFM Cap, na Msaidizi wa Vicar Biju Madhavath, OFM Cap (AP).

08 Agosti 2024, 15:58