Polinesia ya Kifaransa:Makatekista na wahudumu wa Ekaristi ni muhimu
Na Angella Rwezaula - Vatican
Siku ya Ijumaa tarehe 2 Agosti 2024 usiku, Kanisa kubwa la Maria No Te Hau -Mama Yetu wa Amani katika moyo wa Papeete lilijaa. Moja ya matukio muhimu katika maisha ya kichungaji ya Jimbo kuu ni kuadhimishwa. “Baada ya mwezi wa kufundisha katika 'shule mbalimbali za imani' zilizotawanyika katika mji mkuu wa Polinesia ya Ufaransa, Askofu Jean Pierre Cottanceau, SS.CC., alikabidhi utume rasmi kwa makatekista wapya, makatekista wasaidizi na wahudumu maalum wa Ekaristi. Padre Sandro Lafranconi, wa Shirika la Tume za Afrika (SMA), liliambia shirika la Habari za Kimisionari Fides kutokana na kile ambacho yeye mwenyewe alikifafanua kuwa Jimbo kubwa zaidi ya ‘Mama Kanisa.’ “Hao ndio walei wanaojihusisha kwa ukarimu zaidi katika uinjilishaji na maisha ya kila siku ya Kanisa Katoliki. Ni nguvu hai zinazofanya kazi moja kwa moja kupitia Jimboi hili kubwa.”
Wahudumu maalum wa Ekaristi
Kwa mujibu wa mmisionari huyo alisema kuwa: “Mbali na mapadre ishirini na mashemasi hamsini, ni walei, ambao huanzia kwenye visiwa vya mbali zaidi, Visiwa vya Gambier na Austral, kama mishipa midogo na midogo sana inayoruhusu uenezaji wa imani, inayolishwa sana na Kristo Mfufuka.” Makatekista hao wanaitwa Katekita na wamemaliza mafunzo hayo ya miaka 5. Wasaidizi wa Makatekista au Tauturu Katekita wamemaliza miaka miwili kati ya mitano na Tavini, wahudumu maalum wa Ekaristi, wamefuata mafunzo mengine ya miaka miwili ambayo yanaweza kuwa ya awali kwa miaka 5 kutambuliwa kama Katekita.
Kusimamia Sakramenti
Padre Sandro alielezea shauku ya kusema kwamba tafsiri ya Katekita kama 'katekista' inaweza kuleta makosa. “Katekita wameitwa katika majukumu ya kichungaji yenye upeo mpana zaidi kuliko ule ambao ungekuwa jukumu la sura ya ‘kimaadili’ ya Katekista wa parokia. Kwa hakika, wao husimamia adhimisho la Dominika (Liturujia ya neno pasipo padre na wanatoa maoni yao juu ya Neno la Mungu katika liturujia na kusimamia hata Sakramenti ya Ekaristi inatolewa kulingana na masharti yaliyotolewa Kanisa Katoliki.