Peru:Watu Asilia kufanya mkutano wao wa kwanza na Wamisionari wa Consolata
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Imarisha mazungumzo ya kiutamaduni kwa lengo la kutembea pamoja kuelekea monifue (yaani maisha kamili) na kujenga Kanisa karibu na ukweli wa watu wa kiasilia. Hivi ndivyo wawakilishi wa watu Asilia wa Amazonia ya Peru walipendekeza, walipokusanyika pamoja na wamisionari wa Consolata (IMC) katika Mkutano wa Kwanza wa Watu wa Asilia. Hizi ni taarifa na ujumbe kutoka kwa Wamisionari wa Consolata, wawakilishi wa tume sita za Vikariati ya Kitume ya Mtakatifu José wa Amazonia ambao wanaishi moja kwa moja na watu wa kiasili. Kwa mujibu wa Wamisionari wa Consolata walibainisha kuwa: “Hii ni changamoto iliyoshughulikiwa kwa Makanisa mahalia ambayo yatalazimika kutafakari kila siku na kwa dhati jinsi ya kutembea pamoja na watu hawa hapa na sasa.” Aidha pamoja na baadhi ya wajumbe wa wafanyakazi wa utawala, walikutana, katika kijiji cha Angoteros, ili kubadilishana wasiwasi na uzoefu wa pamoja juu ya jinsi ya kuchukua hatua madhubuti kuelekea chaguo la upendeleo kwa watu wa kiasilia.
Jisikie, jifunze na kutembea pamoja
“Tunafahamu kuwa hili linahitaji ubadilishaji wa maumbo, mbinu, nyakati, midundo, lugha na hali ya kiroho,”walibainisha. Vile vile walisema: “Pendekezo la kufanya Mkutano wa kwanza wa Watu wa Asilia pamoja na wamisionari ambao walitaka kwa hiari kuwa sehemu ya mchakato huu liliunganishwa na mada ya: jisikie, jifunze, tembea nao,” kwa pamoja katika kujenga ule utimilifu wa maisha ambao kwa upande wetu umejikita kwenye hali ya heshima na tamaduni mbalimbali.” Kusudi lilikuwa kutoa nafasi ya mazungumzo kati ya tamaduni ambazo zingeruhusu watu kufahamiana, kuthaminiana, kutembea pamoja na kupanda neno la uzima kutoka kwa hekima yao. Watu wa asili 51 wanaishi katika Amazonia ya Peru, miongoni mwao tisa wanapatikana katika Vicariate; Kanisa mahalia ambalo kwa miaka mingi limetembea na kuzunguka pamoja na watu wa kiasili.
Maisha kamili
Kwa mujibu wa Padre José Fernando Flórez Arias, IMC, mmisionari katika Vicariate ya Mtakatifu José wa Amazonia alisema kuwa: “Kwa watu wa kiasilia neno monifue linamaanisha maisha kamili na mkusanyiko huu wa kwanza unawakilisha hii hasa: mavuno ya shamba kubwa lililopandwa kwa aina nyingi ambayo haijawahi kuwakilisha tishio bali ahadi.” Kwa njia hiyo ilikuwa muhimu kuona watu wa Asili waitwao Kichwa wa Ecuador pamoja na wale wa Peru; Murui wa Colombia pamoja na Murui–Uitoto wa Peru” "Mataifa ya kitaifa yalitaka kugawanyika, lakini hawakuweza kuvunja hali ya kiroho ya watu wenyewe. Na hii pia inawakilisha wito kwa Makanisa yaliyoitwa kutembea pamoja, kukutana na kutambuana. Katika Amazonia hili sio suala la kuwa huko lakini kujua jinsi ya kuwa huko. Eneo linahitaji wamisionari wenye furaha, walio wazi kwa kusikiliza, kwa neno, kwa fumbo. Sinodi ya Amazonia, iliyoadhimishwa mnamo Oktoba 2019, ilipendekeza njia mpya katika uhusiano kati ya Kanisa Katoliki na eneo, tamaduni na maisha ya wazee. Kwa hiyo ni muhimu kutembea na vigezo vya Papa Francisko ambaye akiwa, huko Puerto Maldonado, aliwaambia wakazi wa kiasili kwamba: “wasaidie wamisionari wenu kuwa kitu kimoja na ninyi.”