Panama:Agosti 19 hadi 22 unafanyika mkutano wa maaskofu na wahudumu wa kichungaji
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Tuko tayari kuwapokea washiriki katika Mkutano wa 10 wa Maaskofu na wachungaji wahamaji kutoka mikoa ya Amerika ya Kati, Caribbean na Amerika Kaskazini, ambapo tutaendelea na kazi yetu ya kuandamana na wahamiaji na wakimbizi.” Hayo yalisemwa na Askofu Mkuu José Domingo Ulloa Mendieta, wa Jimbo Kuu katoliki la Panama, akitangaza mkutano huo kufanyika huko Panama, kuanzia tarehe 19, hadi Alhamisi tarehe 22 Agosti 2024.
Kuheshimu kanini za nchi
Askofu Mkuu Ulloa alisisitiza kuwa ni jambo la dharura kwa Kanisa Katoliki katika bara hilo, kwa kuzingatia utata wa mgogoro wa wahamiaji, kuwa na ledsagas muundo, na vigezo wazi kwa ajili ya hatua ya kichungaji, kuheshimu kanuni za nchi za wenyenyeji, lakini juu ya yote kuhakikisha kwamba “haki za binadamu za wahamiaji na wakimbizi ni uhakika. Kutembea pamoja na wahamiaji na wakimbizi ni kauli mbiu inayohuisha mkutano huo, ikihamasishwa na Jumuiya ya Kijamii na Kichungaji ya Uhamaji wa Binadamu ya Amerika ya Kati na Caribbien na Huduma ya Kichungaji ya Uhamaji wa Binadamu wa Baraza la Maaskofu wa Panama na Jimbo kuu la Panama.
Katika mkutano anaudhuria Kardinali Czerny
Katika Mkutano huo anashiriki Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu ambaye ameongoza misa Takatifu tarehe 20 Agosti 2024 katika Kanisa kuu la Maria wa Antigua majira ya jioni. Tukio hili la kikanisa linaungwa mkono na Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu, kwa lengo la “kutengeneza nafasi pana ya ushiriki, ili kutoa majibu mapana kwa changamoto za kichungaji zinazoletwa na hali ya uhamiaji katika kanda hizo.”