杏MAP导航

Tafuta

Nicaragua inaendelea na kufukuza watu wa kidini. Nicaragua inaendelea na kufukuza watu wa kidini.  (ANSA)

Nicaragua imewafukuza mapadre 7 sasa wako Roma

Baada ya kukamatwa kwa siku za hivi karibuni,serikali ya Nicaragua iliwafukuza watu mapadre na sasa wako Italia.

Vatican News

Jumatano iliyopita tarehe 7 Agosti 2024, mapadre saba waliokuwa kizuizini huko Nicaragua walihamishwa na kuletwa jijini Roma, ambako walifika tarehe 8 Agosti 2024. Hawa ni Padre Víctor Godoy, Jairo Pravia, Silvio Romero, Edgar Sacasa, Harvin Torres, Ulises Vega, Marlon Velazquez. Habari hizo zilithibitishwa na serikali ya Nicaragua katika taarifa kwa vyombo vya habari: “Mapadre saba wa Nicaragua waliondoka Nicaragua kwenda Roma.” Mapadre hao ni wa Majimbo za Matagalpa na Estelí na walikuwa wamezuiliwa katika Seminari ya Mama Yetu wa Fatima huko Managua.

Wakati huo huo, Balozi wa zamani wa Nicaragua katika Umoja Shieika moja la  Mataifa la Marekani, Arturo McFields Yescas, alithibitisha Jumatano 7 Agosti 2024 kwamba serikali inayoongozwa na Daniel Ortega imeamuru kufukuzwa kwa balozi Breno de Souza Brasil Días da Costa, wa Brazil nchini Nicaragua, kwa kutoshiriki katika maadhimisho ya miaka 45 ya Mapinduzi ya Sandinista mnamo Julai 19, ambayo alikuwa amealikwa. Kwa upande wake, serikali ya Brazil iliamua siku ya Alhamisi  8 Agosti 2024 kumfukuza Balozi wa Nicaragua, Fulvia Castro, kwa usawa, kwa hatua kama hiyo iliyopitishwa na mamlaka huko Managua.

10 Agosti 2024, 14:40