杏MAP导航

Tafuta

Padre Francesco Patton(OFM)Msimamizi wa Nchi Takatifu huko Yerusalemu. Padre Francesco Patton(OFM)Msimamizi wa Nchi Takatifu huko Yerusalemu. 

Nchi Takatifu,Patton kwa vijana:Tuvunje mnyororo wa chuki kwa kutazama Yesu Msalabani

Kuanzia Agosti 16 hadi 18,2024 huko Nazareti ulifanyika mkutano wa vijana ili kuomba na kuishi uzoefu wa kushiriki pamoja kwa kuongozwa na mada:Ninaishi na Wewe.”Msimamizi wa Nchi Takatifu,Padre Patton(OFM),alizungumzia“ujumbe wa matumaini uliozinduliwa na vijana hawa waliofanikiwa kukutana kwa siku chache kuwa pamoja,kutafakari pamoja juu ya maana ya kuwa Wakristo na kupata wakati wa udugu."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

“Ninaishi na Wewe”: Ilikuwa ni mada ya mkutano uliowaona vijana 150 pamoja kwa siku tatu, kuanzia tarehe 16 hadi 18 Agosti 2024 huko Nazareti Nchi Takatifu  kuomba na kuishi uzoefu wa kushiriki. Tukio la mwaka huu, kwa sababu ya mzozo unaoendelea na hali isiyo na utulivu, uliandaliwa na  Wafransiskani tangu mwezi Machi mwaka huu.  Katika tovuti ya Nchi  akatifu inayoripoti habari hiyo, msimamizi wa Nchi Takatifu, Padre Francesco Patton(OFM), alizungumzia: “ujumbe wa matumaini uliozinduliwa na vijana hawa waliofanikiwa kukutana kwa siku chache kuwa pamoja, kutafakari pamoja juu ya maana ya kuwa Wakristo na kupata wakati mkali wa udugu. Nazareti ni mahali pa Umwilisho unaotukumbusha kwamba ni Mwana wa Mungu aliyechagua kuishi nasi: si hivyo tu, bali pia kuishi kwa ajili yetu, yaani, kutoa uhai wake kwa ajili yetu."

Tuvunje minyororo ya hasira na chuku kwa kutazama Yesu Msalabani

Daima na tunavunja mnyororo wa hasira na chuki ikiwa tunaweza kumtazama Yesu Kristo msalabani kwa sababu ni Yesu Kristo msalabani ambaye alichukua maovu yote ya ubinadamu na historia. Uovu ni kama mlipuko wa nyuklia, husababisha athari ya mnyororo na kukatiza mtu lazima awe na ujasiri wa kutojibu. Yesu Kristo pale msalabani alitufundisha kwamba ili tusitende na kuushinda uovu ni lazima tukubali hata kufa, kutoa uhai wetu. Wainjili wa kwanza wa ulimwengu wa vijana ni vijana wenyewe kwa hivyo ikiwa vijana wa siku hizi wanakaribisha neno kwa ujasiri na kuchukua kwa dhati dhamira ya kulimwilisha, watalisambaza pia kwa vijana wengine, wataweza kufanya uchaguzi wa maisha kulingana na Injili na wataweza kutazama wakati ujao kwa ujasiri na bila woga,” alihitimisha.

Siku tatu za kushiriki udugu kwa kuabud, burudan na kukesha kiroho

“Ilikuwa vigumu sana kwetu mwaka huu kuandaa upya maandamano ya Wafransiskani  ambayo hayakuweza kufanyika katika hali yake ya kawaida,” anaeleza Ndugu Mdogo  George Haddad, aliyehusika na tukio hilo pamoja na ndugu wengine na watawa 10 kutoka mashirika mbalimbali “kutokana na mazingira ambayo Nchi yetu imekuwa hai kwa takriban mwaka mmoja, ambapo kila mmoja wetu amehusika. Lakini hii haikutuzuia kuandaa mkutano wa Wafransisko na vijana. Siku tatu za mikutano, kushiriki, burudani, kuabudu na kukesha kiroho zilifikia kilele kwa misa ya mwisho iliyoongozwa na Ndugu Mdogo Padre  Ibrahim Sabbagh, (OFM), Paroko wa Nazareti.

Vijana huko Nazareth wafanya mkutano 16-18 Agosti 2024
22 Agosti 2024, 15:48