杏MAP导航

Tafuta

Coventi Takatifu ya Assisi. Coventi Takatifu ya Assisi. 

Assisi:Mashemasi,manabii na wapanzi wa matumaini katika Warsha la XXIX la Kitaifa

Tangu tarehe 5-8 Agosti 2024,linafanyika Warsha kwa ajili ya maaskofu mashemasi,mapadr,watawa wa kike na kiume pamoja na walei katika mji wa Umbria lililoandaliwa na Jumuiya ya Mashemasi nchini Italia kwa ushirikiano na Uinjilishaji na Harakati ya Laudato si’ambapo linakuza masuala ya sasa,kwa kuzingatia amani na wanawake.

Vatican News.

Wakimbizi, watu maskini, sayari na amani ni mada nne za kuzingatia zitakazoibuka na kuongoza Warsha la Kitaifa la XXIX lililohamasishwa na Jumuiya ya Mashemasi nchini Italia kwa ushirikiano wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji na Jumuiya ya Laudato si’, huko Assisi kuanzia tarehe 5, hadi Alhamisi tarehe 8 Agosti 2024. Kauli mbiu ya mkutano huo: “Mashemasi, manabii na wapanzi wa matumaini”. Washriki ni Maaskofu, mapadre, mashemasi na watahiniwa, watawa kike na kiume na walei watu wa Mungu.

Matumaini, unabii na sinodi

Waliofungua tukio hilo alasiri tarehe 5 Agosti walikuwa ni Askofu Francesco Savino, wa Cassano ya Ionio na makamu rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia, na Enzo Petrolino, rais wa Jumuiya ya Mashemasi wa kudumu nchini Italia. Vipindi vitatu vya kazi vilipangwa: “Ushemasi  na unabii”, katika kuchunguza njia za mabadiliko, na “Ushemasi na sinodi”, kwa mustakabali tofauti na ushemasi wa matumaini ya sinodi. Miongoni mwa wazungumzaji pia watakaozungumza katika siku hizi, ni  Askofu Mkuu Rino Fisichella, Mwenyekiti Mwenza wa  Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, ambaye alitoa hotuba ya utangulizi, Kardinali Pierbattista Pizzaballa, Patriaki wa Yerusalem wa Kilatini, ambaye atazungumza juu ya mada ya amani Jumatano 7 Agosti asubuhi, na Denis Mukwege, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel mnamo 2018.

Msisitizo kwa mwanamke

Katika kumulika suala la wanawake siku ya Jumatano tarehe 7 Agosti 2024 alasiri, miongoni mwa wengine, atakuwa ni Simona Segoloni, makamu  rais wa Uratibu wa Wataalimungu nchini Italia, ambaye atazungumza juu ya “Ukuu wa ushemasi wa nyumbani. Kutoka katika mkutano na maharusi"; kisha kutakuwa na Cristina Simonelli, profesa wa Historia ya Kanisa na Taalimungu ya Uzalendo, kuzungumza juu ya “Kanisa la Kishetani: kutoka hadi kupanda tumaini”; Sista Veronica Donatello, mkuu wa Huduma ya kichungaji kwa watu wenye ulemavu, wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI) na Veronica Coraddu, mratibu wa Kiitaliano wa Wahuishaji na Mizunguko ya Laudato Si' ya Harakati ya “Laudato Si” Ripoti ya mwisho imekabidhiwa kwa Padre  Alphonse Borras, mtaalimungu wa Jimbo la Liège, kuhusu “Uso wa kishemasi wa Kanisa la Sinodi.”

06 Agosti 2024, 16:13