Angola:Huambo ni eneo lililopuuzwa na kuna changamoto za imani za kishirikina
Na Anastacio Sasembele – Luanda, Angola
Huambo ni mkoa wa Angola ulio katika Mkoa wa Kati takriban kilomita 450 kutoka mji mkuu, Luanda. Askofu mkuu Zeferino Zeca Martins, S.V.D, ambaye amekuwa msimamizi wa Kanisa huko Huambo kwa miaka sita iliyopita, ameshirikisha habari na Vatican News baadhi ya changamoto zinazolikabili Jimbo kuu. Askofu Mkuu huyo anaamini kwamba mamlaka hata hivyo inaweza kufanya mengi zaidi kwa eneo hilo katika mambo ya ndani ya Angola.
Zawadi ya mapadre wa jimbo na waseminari
Vile vile, kukiwa na takriban mapadre 150 wa jimbo, 19 kati yao wanatoka nje ya Angola, Askofu Mkuu Zeca alisema bado kunahitajika mapadre wengi zaidi.“Mapadre ni kama lulu; kadiri unavyokuwa na vingi ndivyo unavyohitaji zaidi.” Katika kipindi cha miaka sita iliyopita Askofu mkuu Zeca aliwapa daraja la Upadre zaidi ya mapadre 45 wa majimbo, kwa wastani wa mapadre 8 hadi 10 kwa mwaka. Walakini, uwezo wa kiuchumi wa Jimbo kuu ni changamoto, bila kujali ukarimu wa watu. Uchumi uliodorora, kwa upande wake,ambao unaweka mkazo mkubwa wa kifedha linapokuja suala la kutunza seminari tatu katika Majimbo. Ni mzigo mgumu, kutokana na rasilimali chache zizotokana na mzozo wa kiuchumi na kifedha nchini humo alisema. Askofu Mkuu hata hivyo alishukuru kwa msaada ambao Jimbo kuu linatoa kwa seminari za jimbo. Hata hivyo, kutokana na mahitaji yaliyopo, kiasi kilichotolewa na Vatican hakitoshi. Anaomba msaada zaidi kutoka kwa watu wenye mapenzi mema na wafadhili. Jimbo kuu la Huambo ni mojawapo ya majimbo machache katika Baraza la Maaskofu la Angola na São Tomé (CEAST) ambalo lina seminari zake: seminari ndogo, falsafa na taalimungu.
Imani katika ushirikina huzuia uinjilishaji
Askofu Mkuu Zeca pia alizungumza juu ya hitaji la kubadilisha imani za kiutamaduni za watu kuhusiana na mawazo potofu ya uchawi(Ushirikina). “Hii imeleta changamoto kubwa za kichungaji. Imani ya ushirikian imeenea katika jamii ya Angola na ni chanzo cha wasiwasi na kikwazo cha uinjilishaji katika Jimbo kuu,” Askofu Mkuu alisisitiza. Tangu wakati huo ametoa wito wa mabadiliko makubwa katika fikra. “Uzushi wa imani na utendaji wa uchawi ni bahati mbaya. Inaonesha kuwa hatujaacha utamaduni wetu. Kwa sababu hii, hitaji la uinjilishaji wa kimsingi, katika hali zingine, ni muhimu,” alisema Askofu Mkuu Zeca.
Mkoa wa Huambo unahisi kupuuzwa
Askofu Mkuu wa Huambo alielezea zaidi hali ya kushangaza ya kijamii katika mambo ya ndani ya Jimbo la Huambo, huku watu wakikabiliwa na hali ngumu ya kijamii na kiuchumi. Kwa ujumla, Askofu Mkuu alisema, Serikali ya Angola imepuuza na kutelekeza mambo ya ndani ya Jimbo la Huambo, jambo ambalo limeibua changamoto kubwa za kiuchumi na kijamii kwa wananchi. Hakuna barabara, shule hazitoshi, huduma duni za afya, ukosefu wa usafiri wa kutosha, na kutopatikana kwa huduma nyingine muhimu za kijamii. Askofu Mkuu Zeca anaamini kuwa serikali inapaswa kusambaza rasilimali kwa usawa katika maeneo yote ya nchi.