Kenya kwa ajili ya kusikiliza kilio cha Dunia na maskini
Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.
Kabla ya janga, watu maskini wa kutisha ulimwenguni walikuwa ni zaidi ya milioni 700. Lakini sasa tishio limetolewa na Umoja wa mataifa, kuwa mwishoni mwa mwaka 2021, ipo hatari ya kufikia watu maskini milioni 900. Afrika peke yake inawezekana kuongezeka sana hadi milio 25. Hii ni kwa sasabu, barani Afrika kuna matatizo makubwa ya umaskini wa kutisha, si tu kuzungumza kipeo cha ardhi bila kuzungumza kile cha maskini. Waraka wa Laudato si wa Papa unatoa msukumo wa kutunza maskini na zaidi ndani yake kushughulika katika mitaa yao hasa anapotunza mazingira ambayo pia hawezi kusahau sehemu ya jamii yake. Amesema hayo Padre Benedict Ayodi, ambaye ni Ndugu Mdogo mkapuchini kutoka Nairobi, Kenya, na mhusika wa Harakati Katoliki Ulimwengun kwa ajili ya kudhibiti mabadiliko ya Tabianchi (Gccm), akitafakari juu ya Waraka wa Papa Fracisko wa Laudato sì aliouandika mnamo 2015.
Kama Harakati Katoliki ulimwenguni kwa ajili kuthibiti mabadiliko ya tabianchi, anamesema wanapeleka mbele hawali ya yote mipango ya kulinda msitu nchini Kenya wa Kakamega ambao amesema ndugu Mdogo kuwa leo hii ndio msitu pekee wa mvua uliobaki Afrika Mashariki. Msitu huu umetanda zaidi ya kilomita za mraba 200 na sio mbali na Ziwa Victoria. Katika pafu hili la kijani ambalo ni eneo lenye msitu na kuharibiwa, wamepanda zaidi ya miti elfu tatu ya asilia, shukrani kwa Waraka wa Laudato si, lakini pia hata kwa njia ya jumuiya mahalia, maparokia, na hali halisi nyingine, kwa kushirikishana na waaanglikani wakati wa kipindi cha Kazi uumbaji na hali halisi nyingine ambao nao wwana mipnago inayofanana na washirika wengine ambao wamepanda zaidi ya miti 50,000.
Ni mpango ambao unaunganishwa na ule wa Siku ya Kimataifa ya Misitu 2021 ambayo Umoja wa mataifa umeadhimisha tarehe 21 Machi, kwa kuongoza na kauli mbiu: Kurejeshwa kwa misitu, njia ya kupona na ustawi, kwa namna ya kukemea jinsi kila mwaka ulimwenguni zaidi ya hekta milioni 10 za misitu hupotea zote. Na pia kuangazia Siku ya Dunia ambayo mwaka huu, itaadhiishwa Alhamisi tarehe 22 Aprili 2021 ambayo imechaguliwa kuongozwa na kaulimbiu “Rejesha Dunia Yetu”. “Restore Our Earth”.
Kablya kujiunga na Harakati hii Gccm mnamo 2015 mara baada ya kuchapishwa kwa Waraka wa Laudato Si, Padre Ayodi alikuwa mkurugenzi wa Tume ya Haki na amani na ufungamanishwaji wa kazi ya uumbaji kwa upande wa Shirika la mapadre wakapuchini, Roma tangu 2014 hadi 2019. Yeye asili yake ni kutoka Kakamega nchini Kenya inayopakana na Uganda, na kwa maana hiyo anajua vema msitu wa mvua. Ni kama ule wa Amazonia, ambao ni muhimu sana, kwa kanda hii na kwa Afrika nzima kwa ujumla katika kuweka usawa wa baioanuai na kwa ajili ya kukabiliana na matatizo ya kuongezeka kwa joto la dunia.
Akiendelea kueleza hali halisi mtaalamu wa harakati katoliki kwa ajili ya tabia nchi, amesema Afrika ni moja ya Bara ambalo liko wazi zaidi kwa athari za mabadiliko ya tabianchi na uchafuzi wa mazingira, na ulioongozwa na athari za janga la sasa la Covid-19. Harakati ya Gccm inaona tishio la kuishi kwa watu waafrika kuongezeka kwa ngazi ya maji katika Ziwa Voctoria, Baa la njaa, uvamizi wa nzige kama ambao unaendelea katika sehemu mbambali mbali za pembe ya Afrika mashariki.
Tangu kipindi cha baridi kilichopita wanaendelea kuhamasisha kwa upya kampeni ya kufanya uelewa dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Umakini pia unahusu Bomba la mafuta la Afrika Mashariki (EACOP)“East african crude oil and gas pipeline”,lenye urefu wa kilometa 1,445 ambalo litafirisha mafuta ghafi kutoka Kabale, Uganda hadi peninsula ya Chongoleani karibu na bandari ya Tanga nchini Tanzania ambao tayari umesainiwa mkataba huo. Kama Harakati Katoliki Ulimwenguni kwa ajili ya Tabianchi, amesema wanayo shughuli ya huduma wa utetezi kwa ajili ya Kanisa la Uganda na Tanzania, ili kuwasaidia watu, kwa mfano, kupitia mkutano kwa njia ya mitandao ili kujua matokeo juu ya hali kama hiyo ambayo ambayo baadaye itaweza kuongeza uzalishaji wa kaboni ( yaani hewa chafuzi).
Na zaidi, ameendelea kusema kuwamba mbele labda itawezekana mafuta kuvuja na wakati huo uwezekano mkubwa wa kumwagika kutoka kwenye bomba la mafuta hasa kwa sababu karibu theluthi moja ya muundo huo itajengwa kupitia mpakani mwa Ziwa Victoria, na ambalo ni eneo lenye matetemeko ya ardhi. Na zaidi ya hayo kuna hatari ya mkusanyiko wa takataka za hatari iliyo na benzini ambazo lazima zitolewe kwenye bomba na lisafishwe mara kwa mara. Kwa maana hiyo Mpango huo kwa mujibu wa Padre anasema ardhi za watu zimechukuliwa nchini Uganda na Tanzania. Awali ya yote kuna suala la ukosefu wa haki. Adhi ambazo wamelipwa fedha kidogo na hatari ya kuhamishwa kwa watu. Na kwa upande wa mtazamo wa mazingira ipo hofu kubwa kwa mbuga za hifadhi katika Kanda za Maziwa makubwa na kwa ajili ya wanyama wanaoishi ndani mwake. Misitu mingi tayari umeharibiwa katika Nchi hizi mbili.
Njia kwa ajili ya uongofu wa kiekoloja inapitia hata katika matendo mahalia. Padre amesema kuwa wao wameanzisha makundu madogo madogo yaitwayo mizunguko ya Laudato si, kwa ngazi ya kipatokia nchini Tanzania, Uganda na nchi nyingine barani Afrika. Kwa ushirikiano na Caritas au hali nyingine ya kutoa msada ya Kijesuit, au Wakauchini, wanafanya kazi kwa karibu na watoto wa mitaani katika mtaa wa mabati wa Kibera au katika mitaa mingine mibovu ya Nairobi, ambayo Padre Ayoid anatoa umakini wake akififikiria madeni makubwa ya kijamii, ya uliwengu kuelekea walie ambao wako hatarini na ambao wanaoneshwa wazi katika Waraka wa Laudato Si 2015. Kwa kuhitimisha anasema wanatafuta kuwapatia kila siku chakula, lakini hata kuhamasisha uwezeshaji wa wanawake, na miradi ya shughuli za biashara ndogo ndogo.