杏MAP导航

Tafuta

2021.03.05 Ziara ya kitume ya Papa Francisko nchini  Iraq akiwa na Waziri Mkuu 2021.03.05 Ziara ya kitume ya Papa Francisko nchini Iraq akiwa na Waziri Mkuu  

Hija ya kitume ya Papa Francisko nchini Iraq:Sala ya Jumuiya ya Mt.Egidio

Ni ziara ya kidugu ambayo inapata mwangwi wake katika Waraka wa Fratelli tutti Papa anaelekea huko kama kaka kati ya kaka,kwa maana hiyo ataacha ujumbe mkuu katika nchi hiyo ambayo imeteseka kwa sababu ya vita,vurugu na ugaidi.Ni maneno ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio,akizungumzia juu ya maombi yaliyofanyika katika mkesha,Alhamisi Machi 4,kumsindikiza Papa katika ziara yake ya Kitume,Iraq tarehe 5-8 Machi 2021.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Katika ziara ya 33 ya Papa Francisko nchini Iraq, Jumuiya ya Mtakatifu Egidio imeungana katika hatua zake kwa kufanya mkesha wa sala kwa njia ya mtandao siku ya Alhamisi tarehe 4 Machi 2021. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Jumuiya hii amesema kuwa zira yake ya kitume ni ya amani katika nchi ambayo imegubikwa na vita na ugaidi. Sala zao katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Trastevere Roma zimeongozwa na nyimbo, tafakari na hasa maombi kwa Mungu ili Papa aweze kutumiza utume huu mgumu. Walio wengi wa jumuiya hiyo walifuatilia sala kwa njia ya  mtandao moja moja, kutokana na kuendelea kutunza umbali kwa sababu ya maambukizi ya janga la sasa.

JUMUIYA YA MT. EGIDIO KATIKA KANISA LA MT. MARIA HUKO TRASTEVERE
JUMUIYA YA MT. EGIDIO KATIKA KANISA LA MT. MARIA HUKO TRASTEVERE

Rais wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Bwana Marco Impagliazzo, katika mahojihano na Vatican News amesisitizia, safari hii ya kihistoria ya Mfuasi wa Petro katika Nchi ya Ibrahimu na kusisitiza nguvu za Papa katika kuunda uhusiano wa kidugu ambao ndiyo njia pekee ya kuondokana na migogoro na vita. Ni ziara muhimu na ambayo kwa hakika ni ya amani. Papa anazungumza moja kwa moja kama mwanahija wa mani, na leo hii suala kubwa na ombi  kwa Mungu kwa ajili ya Iraq ni amani ya kudumu. Ni ziara ya kidugu ambayo inapata mwangwi wake katika ‘Waraka wa Fratelli tutti’, yaani Wote ni ndugu. Bwana Impagliazzo amesema kuwa, Papa anaelekea huko kama kaka kati ya kaka na kwa maana hiyo ataacha ujumbe mkuu katika nchi hiyo ambayo imeteseka kwa sababu ya vita, vurugu na ugaidi.

Akiendelea na ufafanuzi wake amesema  Papa ni sura ambayo inajulikana ulimwengu wote kama mtu wa amani  mbali na dini au ubora, na sababu zaidi ya dini. Yeye amekuwa hivyo na ni Papa ambaye katika kipindi hiki kiukweli amesuka uhusiano wa ulimwengu wa kiislamu kuanzia na ule uhusiano kibinafsi na Imam Mkuu wa Al-Azhar, Ahmad Al-Tayyeb, walipotia pamoja ile saini ya makubaliano katika Hati huko Abu dhabi na ziara ya Ayatollah Ali Al Sistani nchini Iraq, ambaye ni kiongozi mkuu wa Waashia. Hayo yote yanafanya utambue kama Kanisa Katoliki la Mtaguso bado leo hii halijaacha kufanya kazi katika uundaji wa mahusiano ya kidugu. Kwa upande mwingine tunaona sehemu mbali mbali za ulimwengu wa kiislamu unatupilia mbali  mizizi ya kila aina ya itikadi na vurugu, amesisitiza mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio

05 Machi 2021, 12:59