Ziara ya Papa,Iraq:ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 150 wa CUE
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji, limezindua Mpango nchini Iraq kwa ajili ya kusindikiza Papa Francisko katika ziara yake ya kitume inayotarajiwa kufanyika nchini nchini Iraq, ijumaa tarehe 5 hadi 8 Machi 2021. Huu ni mfuko wa kisheria wa kipapa ambao utafadhili mafunzo kwa wanafunzi 150 wa Chuo Kikuu katoliki cha Erbil (CUE), mji mkuu wa Mkoa unaojitegemea wa kikurdi nchini Iraq, kwa ajili ya miaka minne ili kuhamasisha muungano kijamii kati ya jumuiya tofauti za kidini na kuwahakakikishia wanafunzi wakristo ubora wa matarajio ya kazi.
Mpango huo una thamani na Euro milioni 1,5. Sehemu kubwa ya wanafunzi wa chuo kikuu ni wakimbizi au waliorundikana ndani ambao wanaotoka katika sehemu mbali mbali za Iraq, miongoni mwao ikiwa ni Baghdad, Basra, Diala, Duhok, Kirkuk, Ninive/Mosul, Sinjar na Sulaimaniya. “Ni ukweli Chuo Kikuu Katoliki cha Erbil kinawakilishwa na muonzi wa mwanga na ishara ya matumaini maalum kwa ajili ya kizazi cha vijana”. Amethibitisha hayo Askofu Mkuu Bashar Warda, wa kikaldayo huko Erbil na mwanzilishi wa Chuo Kikuu hicho. “Kwa msaada wa kifedha, Chuo Kikuu hicho kwa njia ya ufadhili wa masomo utawahakikisha msaada mkubwa na wakati huo huo utawakilisha ishara kubwa ya mshikamano mbele ya wakristo na watu walio wachahche ambao wamebaguliwa katika kanda hii” amesisitiza Askofu Mkuu huyo.
Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Warda, lazima kuwapa habari njema watu wote wakati wa ziara ya Kitume ya Papa na kuweza kutangaza matarajio ya kuwa na wanafunzi elfu moja kufikia mwaka 2025 , kwa kuwahakikishia ukweli wa wakati ujao wa vijana na wazazi wao, na kutoa matumaini mkubwa. “Tunaamini kuwa mpango huu unaweza kuunga mkono ujumbe wa Papa wa mshikamano kijamii na upatanisho”, amesema Thomas Heine-Geldern, rais mtendaji wa Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji. Chuo Kikuu kimeundwa karibu na Wakristo asilimia 72%, Waislamu 10% na 18% ya Yazidi”.
Naye Rais wa Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji amesema kuwa Chuo Kikuu ni mpango muhimu sana kwa ajiliya wakristo ambao wanataka kubaki nchini Iraq Kaskazini na huku Kurdistan. “Wakristo wasingefikiria kuachana na taifa lao ikiwa hawatahisi kubanwa na nguvu zilizo nje ya uwezo wao. Ikiwa vijana Wakristo watapewa fursa ya kupata malezi mazuri watakaa. Shirika la Kipapa la Kanisa hitaji (ACS ) tayari limefanya kila linalowezekana kuwasaidia kukaa nyumbani kwa kuwekeza katika ujenzi wa nyumba zao, makanisa na miundombinu. Sasa ni wakati wa kuanza mpango huo, ambao ni mkubwa sana kwetu, na kuwekeza kwa vijana wa nchi ”.
Kulingana na Alfredo Mantovano, rais wa ACS nchini Italia, amesema “huko Kurdistan ya Iraq, wakristo wachache wanaishi katika muktadha wa ukosefu wa usalama kwa sababu ya hisia ya kutokuwa na utulivu inayosababishwa zaidi ya yote na hali mbaya ya uchumi. Hii inaleta shida kwa vijana hasa: kukaa au kuhama. Katika miaka kumi iliyopita, uwepo wa Kikristo umepungua sana na mfuko wa CUE, ilioanzishwa miaka mitano iliyopita, unataka kuwapa vijana fursa ya kukaa katika nchi yao. Hadi sasa, Chuo Kikuu Katoliki cha Erbil ndicho chuo kikuu pekee Katoliki katika taifa hilo, kuna wanafunzi 170, lakini Asofu Mkuu Warda analenga kuongezeka nguvu zaidi ya miaka minne ijayo, shukrani pia kwa msaada wa kifedha wa wafadhili kutoka Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji (ACS).