Hija ya kitume ya Papa Francisko nchini Iraq:Mkutano wa kidini
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Safari ya Ibrahimu ilianzia kutoka Uru, na ambayo ilikuwa ni safari ya kutoka, ambayo ilihusisha kutoa sadaka. Ilibidi aache ardhi, nyumba na jamaa. Lakini, kwa kuacha familia yake, akawa baba wa familia ya watu. Ndivyo Papa Francisko amekumbusha katika mkutano na viongozi wa kidini, Jumamosi tarehe 6 Machi 2021 akiwa katika ziara yake ya kitume, wakati akitoa hotuba yake ya tatu huko Iraq. “Ni muhimu kufanya hija kuelekea sehemu takatifu: ni ishara nzuri zaidi ya tumaini la Mbingu Duniani”, amesema hayo Papa Francisko huku akionesha ishara nzuri ya kurudi kwa mahujaji katika mji huo.
Papa amesema: “Kupenda na kuhifadhi sehemu takatifu ni hitaji muhimu, kwa kumkumbuka baba yetu Ibrahimu, ambaye katika sehemu mbali mbali alimwinulia Bwana madhabahu kuelekea mbinguni”. Patriaki mkuu atusaidie kufanya maeneo matakatifu ya kila chemi chemi ya amani na mkutano kwa wote”. Ndiyo shauku ya Papa Francisko na kuongeza kusema kuwa: “Kuwepo kwetu hapa leo katika nyayo zake kunaweza kuwa ishara ya baraka na matumaini kwa Iraq, na kwa ajili ya Mashariki ya Kati na kwa ulimwengu wote. Mbingu haijachoka Dunia: Mungu anapenda kila mtu, kila msichana na kila mvulana! Tusichoke kutazama angani, kutazama nyota hizi, zile zile ambazo, wakati wake, zilimwangalia baba yetu Ibrahimu”.
Askofu Pompili wa Rieti, Italia amesema Papa Kukutana na Al Sistani ni kama mwangwi wa mazungumzo ya Mtakatifu Francis wa Asisisi na Sultani wa Misri. “Ni mwelekeo wa kidini tu ambao unaoweza kuunda udugu wa kibinadamu, hisia ya kuwa ndugu kama watoto wa Baba yule yule mmoja. Lakini ni kwa nini hili litokee katika wakati huu muhimu kama ilivyokuwa wakati uliopita wa kidini ambapo, dini zilitumiwa kama mgawanyo kwa madhumuni mengine ya kijiografia kuhusiana na uhuru wa kidini. Mkutano kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Al-Sistani ni ishara tofauti na inaibua mtazamo wa mazungumzo ya Mtakatifu Fransisko wa Assisi ambaye, wakati wa Vita vya Kidini vya tano, mnamo Juni 1219, alikwenda kwa Sultan wa Misri, Malek al-Kamel, na ambapo historia hii inatukumbusha kwa njia fulani kwamba uhuru wa kidini umehakikishiwa awali ya yote na uwezo wa watu wa imani kuheshimiana”.
Askofu Domenico Pompili, ametoa maoni yake kuhusu ziara ya Papa kuanzia na mji mkuu wa Iraq, tarehe 5 Machi na asubuhi tarehe 6 Machi ambapo kwenda Najaf kumtembelea kwa faragha Ayatollah Sayyid Ali Al-Husayni Al-Sistani. Katika mkutano wao, Papa amesisitiza umuhimu wa ushirikiano na urafiki kati ya jumuiya za kidini kwani ni katika kukuza heshima ya pamoja na mazungumzo ndipo inawezekana kuchangia wema wa Iraq , wa dini na wa ubinadamu wote, Papa amebainisha.