杏MAP导航

Tafuta

Hija ya kitume ya Papa Francisko Iraq:jengeni jamii juu ya udugu na mshikamano

Katika hotuba ya Papa kwa mamlaka,wafanyakazi wa umma na wanadiplomasia ameonesha njia ya kuelekea kupona kwa taifa kufuatia na miaka ya mizozo na ugaidi.Na Kardinali Sako anaonesha matumaini ya wakati ujao ulio bora kwa wanairaq.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Katika hotuba ya kwanza ya ziara yake ya kitume ya 33  akiwa nje ya Italia, Papa Francisko Ijumaa tarehe 5 Machi 20201 mara baada ya kufika nchini Iraq na kuanza mikutano amebainisha kuwa safari yake nchini Iraq imefanyika katika wakati ambapo ulimwengu unajaribu kutoka katika janga la Covid-19. "Ni mgogoro ambao umeathiri sio tu afya ya watu lakini pia umezidisha hali mbaya ya kijamii na kiuchumi" na kwa maana hiyo anasema "inahitaji juhudi za pamoja za kuchukua hatua ili kuweza kupona kwa pamoja. Lakini zaidi ya yote, mgogoro unatutaka wote tufikirie tena mitindo yetu ya maisha… na kwa maana ya kuishi kwetu"akinukuu katika Waraka wa (Fratelli tutti, 33). Papa ameongezea kusema "ili kuweza kutoka humo tunahitaji kuondoka tukiwa bora kuliko hapo awali, na kwa kuunda siku zijazo kulingana na kile kinachotuunganisha kuliko kile kinachotugawanya".

PAPA AKISALIMIA WALEMAVU
PAPA AKISALIMIA WALEMAVU

Wakati huo huo “Wakristo walikuwa wengi hapo awali na wakati Waislamu walipofika katika nchi yetu, taratibu wao wakaongezeka kuwa mengi. kiukweli babu zetu walionesha na kuunda mfano mwema wa kuishi pamoja, wakichangia sana katika utamaduni; leo  hii tumekuwa wachache, lakini ni wachache ambao ni wachangamfu na wenye bidii na tumechangia ujenzi wa Iraq na maendeleo ya utamaduni wake". Ndiyo Picha halisi ya Patriaki wa Kikaldayo, Kardinali  Louis Raphaël Sako, na rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Iraq, katika hotuba ya kukaribisha Papa katika Kanisa kuu la Kisiro- Katoliki jijini Baghdad.

PAPA AKIWA NA MAASKOFU KATIKA KANISA KUU LA MAMA WA MWOKOZI
PAPA AKIWA NA MAASKOFU KATIKA KANISA KUU LA MAMA WA MWOKOZI

"Katika miaka ya hivi karibuni tumekabiliwa na shida nyingi, hatari na mateso na ushuhuda uli mzuri ni kanisa hili kuu la Wakatoliki wa Siria ambamo tumekusanyika,na kanisa ambalo lilishambuliwa na bomu na waalifu mnamo tarehe 31 Oktoba 2010”, ameendelea kueleza Kardinali Sako. Wakati wa misa takatifu, wafia dini 48 waliuawa, miongoni mwao wakiwemo makuhani wetu vijana wawili, Tha'er na Wasim, na wengi walijeruhiwa. Mnamo Agosti 2014, ISIS iliwafanya Wakristo wote 120,000 kukimbia bonde la Ninawi na Mosul, na tunamshukuru Mungu kwamba maeneo haya yalikombolewa mnamo 2017 na 50% ya wakazi wake wamerudi”. Kardinali  hata hivyo amemshukuru Papa kwa yote kwa sala zake na kujihusisha kwake  na nchi hiyo pia hata mapenzi mema ya watu wa Iraq ambao amethibitisha kuwa wataweza taratibu kuondokana na mgogoro huo ili kufikia wakati ulio bora ujao. 

05 Machi 2021, 16:48