杏MAP导航

Tafuta

2021.01.27 Historia ya Laudato si’ - Papua Guinea Mpya 2021.01.27 Historia ya Laudato si’ - Papua Guinea Mpya 

Papua Guinea Mpya:Njia ya maendeleo endelevu ili kusitisha unyonyaji!

Ardhi ya Papua Guinea Mpya iko katika Bahari ya Pasifiki ambayo ilikuwa ya kwanza kwa shirika la Pime kwenda msafara wa watu 7.Uwepo wao ulikatizwa mnamo 1855,baada ya kuuwawa mfiadini mwenyeheri Giovanni Mazzucconi,na kuanza tena mnamo 1981.Shukrani kwa Mfuko wa 'SI'42',Dada Papua Guinea mpya wamisionari wa PIME wamelenga kukuza mipango ya maendeleo endelevu na zaidi utunzaji wa mazingira.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Njia ya maendeleo endelevu ili kusitisha unyonyaji. Ni dhamana ya karibu inayowaunganisha wamisionari wa PIME, ambalo ni Taasisi ya Kipapa ya Utume wa Kigeni, na mbao kwa upande wa Papua Guinea Mpya wamejikita katika harakati za utume wao. Ardhi hiyo ya Bahari ya Pasifiki ilikuwa yao wa kwanza kwenda katika msafara wa watu 7. Uwepo  wao ulikatizwa mnamo 1855, baada ya kuuwawa mfiadini mwenyeheri Giovanni Mazzucconi,na kuanza tena kwa upya mnamo 1981. Leo kuna watawa 12 nchini humo na wameongezeka Masista 28 wa Shirika la Moyo safi wa Bikiria Maria. Baada ya kutekeleza mipango kadhaa ya maendeleo kwa miaka sasa , wamisionari wa PIME wamechagua kutenga Mfuko wa Nchi wa 2021 kwa ajili ya  Papua Guinea Mpya, mkusanyiko wa michango ambayo katika kampeni za 2019 na 2020 zilikuwa ni kwa ajili ya Amazonia na China. Tafakari iliyowaongoza inaanziakwa Waraka wa Papa wa Laudato si ' ambao, mnamo 2015, ulichukua picha ya Sayari, ukitaka kushinda mipaka fulani ya unyonyaji, bila kutatua shida ya umaskini. Hata hivyo leo hii, karibu miaka sita baadaye, katika nchi nyingine mipaka imefunguliwa kwa unyonyaji wa maliasili, nyingine kati ya hizi ni huko Papua Guinea Mpya

Hayo yamethibitishwa na Giorgio Bernardelli, mhusika wa mawasiliano wa PIME, akizungumza na Vatican News. Kwa mujibu wake amesema kuwa usawa wa mazingira wa nchi ya Pasifiki umepata kuzorota sana katika muongo mmoja uliopita kwa sababu Taasisi ya Kipapa za Utume wa  nchi za  Kigeni, inaeleza kwamba  ni mazoezi yasiyoweza kudumishwa ya matumizi ya rasilimali, ukataji miti hovyo, uharibifu wa makazi ya asili, uchafuzi wa mazingira na utawala mbaya wa eneo hilo. Kwa mujibu wa Bernardelli, ameongeza kusema kuwa ni moja ya maeneo, ambapo uchumi wetu wa ulimwengu hupata wingi wa malighafi tunayohitaji kwa urahisi zaidi: dhahabu, fedha, shaba, madini kwa jumla.

Papua Guinea Mpya ni ardhi tajiri sana kwa mtazamo huu na ni ardhi ambayo pia kuna mipaka mpya ya unyonyaji huo. Moja ya shida kubwa leo hii , ameripoti, ni ile ya uchimbaji mchanga, yaani madini ya uchimbaji wa mchanga. Kuna maeneo yote ya pwani ya Papua Guinea Mpya ambayo yako katika hatari ya kumomonyoka kwa sababu ya unyonyaji wa vifaa hivi kwa usafirishaji. Lakini kuna miradi hata ya uchimbaji wa baharini, kwa maana unyonyaji wa rasilimali chini ya bahari, yaani kwenye bahari, amebainisha. Shukrani kwa Mfuko wa 'S142  yaani Laudato si’, Dada Papua Guinea Mpya', wamisionari wa PIME ambao leo ni idadi yao ni  460 ulimwenguni wanalenga kukuza mipango  ya maendeleo endelevu na shughuli katika maendeo yao ya utume  ambayo ni pamoja na usambazaji wa umeme na maji kwa kutumia mazingira duni zisizo leta athari mbaya ya mazingira.

“Tunataka kukuza mipango rahisi, ya msingi, ambayo huanza kutokana  na maisha ya watu. Mipango ambayo inahusiana hasa na maji: inaweza kuonekana kuwa ya kushangaza lakini sawa kwenye kisiwa katikati ya bahari, kuwa na maji safi inakuwa changamoto ngumu sana katika jamii zingine. Na kwa maana hiyo baadhi ya mipango tutakayokuza inahusu uboreshaji wa maji kama rasilimali ya maisha na pia kwa usawa endelevu kwa muda. Eneo lingine kubwa la kujitoa ni lile ya nishati, kwa  kupitia paneli za jua tunajaribu kuhakikisha upatikanaji wa nishati inayoheshimu rasilimali ”

Pia kuna shughuli nzima ya kukuza uelewa, kwa watoto, vijana na watu wazima, juu ya masuala ya utume na utunzaji wa mazingira. “Mipango ambayo Bernardelli ana nia ya kutaja  kuwa tutafanya huko Papua Guinea Mpya, lakini pia nchini Italia, hasa shuleni. Kwa sababu tunachotaka kuelewa ni kwamba hii siyo historia ya mbali, ambayo inawahusu wale tu walio upande wa pili wa ulimwengu. Ni nini kinachopatikana huko  ni mateso, ubishani na  mara nyingi ni matokeo ya chaguzi ambazo hufanywa ili kuendelea kudhibitisha mtindo wa maisha ambao ndio tunaishi kila siku, bila kufikiria sana juu ya matokeo.

03 Februari 2021, 16:34