Asia:Kardinali Bo awashauri wakatoliki kupokea mwaliko wa Papa ili kushinda majanga mengi!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Ni mwaliko wa kuendelea ambao Papa Francisko anahimizi katika Waraka wake mpya wa “Fratelli tutti”, yaani Wote ni ndugu katika mazungumzo, heshima na ukarimu kwa kila mwanadamu, lakini ambao umesisitizwa kwa mara nyingine kwa wakatoliki wa Asia hata kama wao ni wachache hasa katika kipindi hiki kigumu cha kiafya ulimwenguni. Hayo ndiyo yaliyomo kwenye barua ya Shirikisho la Baraza la Maaskofu barani Asia kwa mujibu wa Kardinali Charles Maung Bo, askofu Mkuu wa Yangon na Rais wa shirikisho hilo, barani Asia (Fabc). Barua iliyotangazwa tarehe 12 Oktoba 2020 ina wito wa nguvu kwa jumuiya zote katoliki ili kuendelea kupokea wito wa Papa wa kuwa na mshikamano, makutano na ukarimu wa kutoa katika kipindi ambacho kwa dhati barani Asia kinajikuta kutetemeka si tu sababu ya virusi, lakini pia hata na majanga mengine. Tafakari ya Kardinali Bo inaanzia na matukio yanaoonesha kuwa mwaka 2020 umekuwa na kipindi cha vurugu, hofu na kupoteza kwa sababu ya virusi vya corona ambavyo vinaendelea kuleta matumaini ya wakati ujao. Pamoja na hayo yote, Papa Francisko anatusahauri kutotoa majibu ya kijujuu tu katika mgogoro huu. Hiki ni kipindi cha kujenga na kuheshimiana, kuishi kama tunavyopendelea kuishi katika ulimwengu ujao.
Kardinali Bo amesema Papa Francisko anatueleza kuwa, kuna ziadi ya janga katika ulimwengu wa sasa. “Ubaguzi wa rangi, ukosefu wa haki, chochezi za chuki, dharau kwa maskini, wazee na watoto ambao hawajazaliwa, usafirishaji wa wanawake na watoto, vyote hivyo viko katikati yetu yaani ndani ya idadi za majanga. "Kila mmoja wenu anafahamu mahali uchungu ulipo ambapo utamaduni wa kifo uko katika Makanisa yenu na katika jamii. Tunajua kuwa karibu nchi 18 za Asia adhabu ya kifo bado ni halali. Tuna biashara ya silaha barani Asia na baadhi ya vita virefu zaidi ulimwenguni. Mamilioni ya watu hawana njia nyingine ila kuacha familia zao na kwenda nje ya nchi kutafuta kazi”. Shida zote tayari ziko katikati ya umakini wa Kanisa ambazo,kwa mujibu wa rais wa Fabc, amesisitiza kuwa "ni muhimu kuhamasisha juu ya chanjo za huruma, mshikamano na haki". Barua hiyo inazingatia mfano wa Msamaria Mwema aliyependekezwa na Papa Fransisko katika sura ya pili ya maandishi: “ kwa kuongozwa na kutafakari juu ya mfano huo, yeye anafuata njia ya pamoja kwaa ajili ya ubinadamu kupitia jitihaza za kujitoa kwa ajili ya amani, kukataa vita na adhabu ya kifo, kutia moyo kwa ajili ya msamaha na upatanisho ndani ya jamii na utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja. Tunapotazama kwa macho yaliyosafishwa na Injili, tutamtambua Kristo katika kila mtu aliyetengwa”.
Jambo lingine ambalo Kardinali Bo anaweka umakini hasa kwa kile kinacho fafanuliwa kwenye nyaraka tatu “Evangelii gaudium”, “Laudato si” na “wote ni Ndugu”. Nyaraka hizi tatu kwa mujibu wa Kardinali Bo anasema, zinakamilishana. 'Evangelii gaudium' anaombea upatanisho na Mungu.' 'Laudato Sì' ni kilio cha moyo ambacho kinaomba upatanisho na kazi ya uumbaji; 'Fratelli tutti' anaomba upatanisho, mazungumzo na mshikamano kati ya wanadamu wote kama dada na kaka. Kama watumishi wa utume wa Kristo leo tunaalikwa kumsaidia katika kuanzisha uhusiano wetu na Mungu, na uumbaji na wanadamu wengine," anaandika askofu mkuu wa Yangon. Ili kutambua udugu wa ulimwengu wote ulioneshwa katika waraka , Kardinali Bo, anarudia maneno ya Papa katika sura ya tano, yasemayo “ni lazima kuwa na sera bora inayolenga wema wa pamoja na ambayo ni pamoja na kwa watu, ambayo ina hadhi ya kibinadamu kama lengo lake na inaunganisha uchumi katika muundo wa kijamii na kitamaduni". Hii ni changamoto inayoihusu bara la Asia kwa namna ya pekee anaongezea “hali halisi yetu ya Asia ambayo inamulikwa na ujumbe wa dharura kuwa 'Fratelli tutti' yaanini 'Wote ni Ndugu'.
Kwa kuhitimisha anasema "Njia tutakayochukua itaamua urithi ambao tutauachia kizazi chetu kijacho, amerudia kusisitiza Kardinali Bo na kwamba Serikali nyingi za Asia zinajaribu kurudi kwenye mitindo ya kiuchumi na kijamii iliyothibitisha na uliyoshindwa, kwa hivyo kuna dharura ya haraka ”. Kufuatia na hli ndipo anahitimisha akiwa na matumaini kwamba ushauri wa Papa kuhusu mshikamano, kukutana na ukarimu unaweza kupata mwangwi katika jamii za Wakatoliki wa Asia: Hata ikiwa sisi ni wachache tu, Papa Franciskp anatuhimiza kusema kwa nguvu kuwa wote ni kama kaka na dada.